Monday 16 April 2018

Wolves Kucheza Ligi Kuu England Msimu Ujao


LONDON, England
VINARA wa Ligi Daraja la Kwanza Wolverhampton Wanderers imepanda daraja na kufuzu kucheza Ligi Kuu ya England msimu ujao baada ya mchezo wao wa juzi.

Timu hiyo imemaliza miaka sita ya kuwa nje ya Ligi Kuu bila ya kucheza wakati wapinzani wao wa karibu Fulham kutoka sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Brentford, ambayo ilisawazisha katika dakika ya 94.

Wolves,ambao wana pointi 92 baada ya kucheza mechi 42, ilikuwa ikihitaji pointi zingine nne kutoka katika mechi zao nne za mwisho ili kushinda taji lakini wamepanda daraja kimahesabu.
Vinara hao wamejihakikishia nafasi hiyo ya kukipiga Ligi Kuu bia utata wowote kufuatia kuwa karibu na wakala wa Kireno Jorge Mendes.

Mendes ni wakala wa kocha mkuu Nuno Espirito Santo na wachezaji nyota Ruben Neves, Diogo Jota na Ivan Cavaleiro. Pia ana uhusiano wa muda mrefu na mmiliki wa klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment