Sunday 29 April 2018

Asikitishwa Mahudhurio Hafifu Mei Mosi 2018


Baadhi ya wachezaji wa timu ya Uchukuzi wakiwa na vikombe vyao 13 walivyoshinda kwenye mashindano ya Kombe la Mei Mosi yaliyomalizika jana mkoani Iringa. (Picha Zote na Bahati Mollel wa TAA).

Na Bahati Mollel-TAA, Iringa
MWENYEKITI wa Tuico Taifa, Paulo Sangeze amesikitishwa na mahudhurio duni yaliyosababishwa na wanamichezo wafanyakazi kunyimwa fursa kushiriki Michezo ya Mei Mosi mwaka huu iliyofanyika mjini hapa.

Alisema kuwa anaungana na waandaaji kushangaa idadi ndogo ya ushiriki katika mashindano ya mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Klabu ya Uchukuzi, Mbura Tenga (kulia) akipokea cheti cha ushiriki wa mashindano ya Mei Mosi yalifanyika  kwenye viwanja mbalimbali mkoani Iringa kutoka kwa mgeni rasmi Mwenyekiti wa TUICO Taifa,  Paul Sangeze.
“Mashirikisho yote ya wafanyakazi tumesikitika kwa idadi hii ndogo na tutahakikisha miaka ijayo timu zinaongezeka zaidi, na tunaipongeza timu ya netiboli ya Ofisi ya Rais Ikulu kushiriki wameonesha mfano mzuri,” amesema Bw. Sangeze.


Pia amesema michezo mahala pa kazi inasaidia kujenga miili ya wafanyakazi na kuongeza tija na bidii kazini, kwani viongozi wasiopenda michezo wanasababisha wafanyakazi kupata magonjwa nyemelezi.

Naye Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Mei Mosi, Bi. Joyce Benjamin alisema Rais John Pombe Magufuli hajawahi kukataza michezo, na inashangaza utashi wa viongozi wasiopenda michezo wanaokataza timu zao kushiriki kwenye michezo.

Mwakilishi wa Gazeti la Uhuru mkoani Iringa, Bi. Ester Malibiche (kulia) akipokea cheti cha ushiriki wa gazeti lake katika michuano ya Kombe la Mei Mosi iliyofanyika kwenye viwanja mbalimbali mkoani Iringa. 
“Tunaomba viongozi wa vyama vya wafanyakazi wa kila eneo la kazi kuingilia kati juu ya hili katika dhana nzima ya wafanyakazi kufanya michezo na kushiriki kwenye michezo ya mashirikisho mbalimbali kama Shimiwi, Shimuuta na kutofanya michezo kunapingana na ilani ya Chama cha Mapinduzi, inayosema wazi juu ya kuinua michezo nchini,” amesema Bi. Benjamin.

Katika mashindano hayo, klabu ya michezo ya Uchukuzi iliyopo (Sekta ya Uchukuzi) imebuka kidedea katika michezo ya michuano ya Kombe la Mei Mosi 2018 baada ya kushinda vikombe 13 vya michezo 10 iliyoshindaniwa kwenye viwanja mbalimbali mjini hapa.
Bi. Sharifa Amir wa Uchukuzi (kulia) akikabidhiwa kombe la ushindi wa kwanza wa mchezo wa draft kwa wanawake kutoka kwa mgeni rasmi Bw. Paul Sangeze ambaye ni Mwenyekiti wa TUICO Taifa. 
Timu hiyo inayoundwa na wachezaji mahiri imeweza kutwaa ubingwa wa kwanza kwa wanaume katika michezo ya mbio za baiskeli (Chaptele Muhumba), draft (Johanson Ngido), bao (Said Omar) na kuvuta kamba, huku kwa wanawake wametwaa ubingwa katika mbio za baiskeli na riadha (Scolastica Hasiri), bao (Sharifa Amir) na draft olnel) na karata wanawake na wanaume (Zamatradi Yusufu na Mosses Machunda).

Timu ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) imeshika nafasi ya pili kwa kujikusanyia vikombe tisa kwa kutwa ubingwa wa soka, riadha wanaume (Lazaro Lugano) huku ushindi wa pili katika michezo ya riadha wanawake (Cartace Manampo), na baiskeli (Happy Mwanga), karata (Sheila Mwihava) na Nkwabi Kadago (mwanaume), na ushindi wa tatu netiboli, Stanley Umbe (baiskeli) na Jackline Massawe (bao).

Timu ya Chuo Kikuu cha Tiba ya Sayansi (MUHAS) wamekuwa watatu kwa kujikusanyia vikombe vitano vya bingwa wa karata wanawake (Emily Kyando), ; mshindi wa pili katika bao (Severina Mnyaga), huku mshindi wa tatu michezo ya kuvuta kamba na baiskeli wanawake (Severina Mnyaga) na dratf (Rebecca Chaula).

Timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wameshika nafasi ya nne kwa kujikusanyia vikombe vinne vya ushindi wa pili katika riadha, baiskeli na bao  wanaume (Michael Luanga),  Nehemiua Johnas na Suleiman Chitanda, huku nafasi ya tatu ya draft ilichukuliwa na Joseph Mlimi.
Nahodha wa timu ya netiboli ya Ofisi ya Rais Ikulu, Bi. Sophia Komba (kulia) akipokea kombe la ubingwa wa mchezo wa netiboli wa michuano ya Kombe la Mei Mosi iliyomalizika jana kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa kutoka kwa mgeni rasmi Bw. Paul Sangeze ambaye ni Mwenyekiti wa TUICO Taifa.
Timu ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu (NAOT) wamejikusanyia vikombe vitatu pekee na kuwa watatu. Vikombe vya ushindi wa pili draft wanawake na wanaume Rosemary Skainde na Alphonce Sika na ushindi wa tatu wa kamba wanaume; nazo timu za Ofisi ya Rais Ikulu, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Geita Gold Mine (GGM) kila mmoja wamejikusanyia vikombe viwili, nazo timu za RAS Iringa na Tumbaku ya Morogoro wote wamepata kikombe kimoja-kimoja.
Nahodha wa mabingwa wapya wa soka wa michuano ya Kombe la Mei Mosi timu ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Stanley Uhagile akikabidhiwa kombe na mgeni rasmi Mwenyekiti wa TUICO Taifa, Bw. Paul Sangeze. Mabingwa wa zamani Geita Gold Mine (GGM) wameibuka washindi wa tatu. 


No comments:

Post a Comment