Tuesday 24 April 2018

Maandalizi Heart Marathon 2018 Yakamilika

Mratibu wa Heart Marathon 2018, Peter Sabuni (kulia) akimkabidhi fulana Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam (DAA) leo, Lukas Nkungu kwa ajili mbio hizo zitakazofanyika Jumapili jijini Dar es Salaam.

   Na Mwandishi Wetu
MAANDALIZI ya mbio za tatu za Heart Marathon zitakazofanyika Jumapili Aprili 29 jijini Dar es Salaam, yamekamilika na kinachosubiriwa ni siku yenyewe ili kumpata mshindi.

Mratibu wa Kamati ya Maandalizi ya Heart Marathon 2018, Peter Sabuni alisema leo kuwa, kila kitu kimekwenda vizuri kwa upande wa maandalizi ikiwemo medali kwa washiriki na watakaomaliza mbio za kilometa 21, 10, tano na meta 700 kwa watoto.

Sabuni alisema mbali na medali pia kamati imeshaandaa fedha taslimu kwa washindi, ambazo kwa ujumla ni kiasi cha Sh milioni 16, ambapo washindi wa kwanza kwa wanaume na wanake katika kiometa 21, kila mmoja ataondoka na kitita cha Sh milioni 2.
Mratibu wa Kamati ya Maandalizi ya Heart Marathon, Peter Sabuni akionesha medali watakaogawiwa washindi wa mbio hizo. 
 Pia fulana kwa washiriki ziko tayari kwa ajili ya washiriki wote, vifaa vya kusomea muda wakati wa kukimbia, namba za washiriki, njia tayari imepimwa kikamilifu kwa kuwatumia wataalam, kutakuwa na usalama wa kutosha kwa wakimbiaji na mambo mengine muhimu.

Alisema kuwa kingine, washiriki wote watapimwa afya zao, watapimwa uzito na urefu, shinikizo la damu, kisukari, wingi wa mafuta mwilini na kupata ushauri wa kitaalam kutoka kwa madaktari.

Alisema kuwa nafasi za kujisajili kwa ajili ya kushiriki mbio hizo bado zipo, ambapo wakubwa wanalipa Sh 30,000 wakati watoto ni Sh 20,000.

Katibu Mkuu wa Chama cha Roadha Mkoa wa Dar es Salaam, DAA, Lucas Nkungu akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Heart Marathon 2018 leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mratbu wa mbio hizo, Peter Sabuni na kulia ni Katibu wa Chama cha Baiskeli Mkoa wa Dar es Salaam (Chabada), Mussa Juma.
Wadhamini wa mbio hizo ni pamoja na Tindwa Medical and Health Service, CBA, Nexlaw Advocates, TCRA, TPB Bank, Sanlam Life Assurance, AGPAHI, AAR, Power Limited, Jamii Forum, Samaki-Samaki, Issa Michuzi Blog, Azania Post.
 
Kwa mujibu wa waandaaji, wanariadha kibao kutoka ndani na nje ya nchi tayari wameshajiandikisha kwa ajili yam bio hizo, ambazo zitaanzia karibu na ufukwe wa Coco, Oysterbayi na kupita katika mitaa mbalimbali kabla ya kumalizikia hapo zilipoanzia.

No comments:

Post a Comment