Sunday 29 April 2018

Liverpool Kumuongezea Mshahara Mo Salah


LONDON, England
KLABU ya Liverpoo inajiandaa kuongezea mshahara Mo Salah ili kumuwezesha kuendelea kuwepo Anfield, imeelezwa.

Kocha wa Liverpool, yuko tayari kuanza mazungumzo ya kumpatia mchezaji huyo kiasi cha pauni 185,000 (sawa na Sh milioni 582) kwa wiki ili kumaliza maswali kuhusu hatma ya mfungaji huyo wa mabao 43 msimu huu.

Makali ya mabao ya Salah umeishtua Real Madrid na kutaka kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri, ambaye hashikiki kwa mabao katika Ligi Kuu ya England.
 
Kwa sasa Salah analipwa kiasi cha pauni 90,000 kwa wiki, ambazo ni sawa na zaidi ya Sh milioni  283 ikiwa na maana kuwa Salah mwenye umri wa miaka 25, hayumo katika orodha ya wachezaji wanaolipwa mishahara mikubwa Liverpool licha ya kuelekea kuipeleka timu hiyo katika fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

Kocha wa Liverpool anataka kukwepa majina makubwa mengine kuondoka katika klabu hiyo kama ilivyokuwa kwa Luis Suarez na Philippe Coutinho ambao walihamia Barcelona.

Liverpool wanaweza kupata mara nne zaidi ya kiasi cha pauni milioni 34.3 walicholipa Roma katika kipindi kilichopita cha majira ya joto wakati Liverpool ilipokuwa ikimnunua mchezaji huyo.

Lakini Liverpool wanataka kumbakisha mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri na kuongeza miaka minne aliyoibakisha katika mkataba wake.

Mkataba mpya wa Salah unatarajia kufanyika kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia wakati thamani yake inaweza kuongezeka zaidi.


No comments:

Post a Comment