Tuesday, 13 June 2017

Ratiba Ligi Kuu England hadharani leo

LONDON, England
RATIBA kamili ya Ligi Kuu ya England msimu wa mwaka 2017-18 itatolewa asubuhi hii, imeelezwa.

Msimu mpya wa Ligi Kuu unaanza Agosti 12 na kwa mara ya kwanza itashirikisha pamoja na timu za Brighton na  Huddersfield, ambazo zimepanda daraja.

Chelsea ndio mabingwa watetezi, wakati Newcastle nayo pia imepanda daraja kutoka katika Ligi Daraja la Kwanza msimu uliopita.
Ligi hiyo inatarajia kumalizika Jumapili ya Mei 13, 2018, wiki moja zaidi ya msimu uliopita, huku fainali za Kombe la Dunia zikitarajia kuanza Urusi Juni 14.

No comments:

Post a Comment