Thursday 4 January 2018

Yanga Hakuna Kulala Mapinduzi Cup Zanzibar, Leo Wanacheza na Taifa Jang'ombe Uwanja wa Amaan

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Yanga leo usiku wanacheza mchezo wao watatu wa Kundi B wa Kombe la Mapinduzi itakapochuana na Taifa Jang’ombe kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

  Mchezo huo utakaoanza majira ya saa 2:15 usiku, unakuja siku moja tu baada ya Yanga kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya JKU jana, bao la dakika ya 90 la beki Hassan Ramadhani Kessy.

Kwa ushindi huo mwembamba, Yanga SC inafikisha pointi sita baada ya mechi mbili, ikiwemo ya kwanza waliyoshinda 2-1 dhidi ya Mlandege juzi na ikishinda leo itakuwa imejihakikishia kwenda Nusu Fainali hata kabla ya mechi zake mbili za mwisho dhidi ya Zimamoto FC Januari 7 na Singida United Januari 8.

Mechi ya kwanza leo itakuwa ni kati ya Mlandege na Singida United Saa 8:30, kabla ya URA kumenyana na Azam FC Saa 10:30 jioni.

Baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi Jamhuri ya Pemba kwenye mchezo wa Kundi A jana usiku, Simba itarejea Uwanja wa Amaan kesho kumenyana na Azam FC Saa 2:15 usiku.

Ushindi wa jana uliotokana na mabao ya mabao ya washambuliaji, Nahodha John Raphael Bocco, chipukizi Moses Kitandu na beki Mghana, Asante Kwasi uliifanya Simba ifikishe pointi nne baada ya sare ya 1-1 na Mwenge SC katika mchezo wa kwanza.


Na baada ya mechi ya kesho dhidi ya Azam FC, Simba watarejea Uwanja wa Amaan Januari 8 kumenyana na URA ya Uganda Saa 10:30 jioni kukamilisha mechi zake za Kundi A.

No comments:

Post a Comment