Monday 15 January 2018

Paul Lambert ndiye kocha mpya Stoke City

LONDON, England
STOKE City imemteua kocha wazamani wa Aston Villa na Norwich Paul Lambert kuifundisha timu hiyo, imeelezwa.

Raia huyo wa Scotland mwenye umri wa miaka 48 ametia saini mkataba wa miaka miwili na nusu wa kuifundisha timu hiyo.

Atachukua mikoba ya Mark Hughes aliyetupiwa virago mwezi uliopita.

Stoke City katika msimamo wa Ligi Kuu ya England wako katika nafasi ya 18, ambapo wanahitaji pointi moja tu ilikuweza kujinasua kutoka kutoka katika hatari ya ukanda wa kushuka daraja. Waliondolewa katika Kombe la FA baada ya kuchapwa na Coventry City.

Mechi yake ya kwanza kwenye usukani itakuwa mechi ya nyumbani dhidi ya Huddersfield Jumamosi.

Lambert amekuwa bila kazi tangu kuondoka katika klabu ya Wolves mwishoni mwa msimu uliopita.

Amewahi kuwa mkufunzi Colchester, Wycombe Wanderers na Blackburn.

Alipokuwa mchezaji, alishinda mataji ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya akiwa na Borussia Dortmund mwaka 1997 na akashinda mataji manne ya ligi nchini Scotland akiwa na Celtics.


Aliichezea timu ya taifa ya Scotland mechi 40.

No comments:

Post a Comment