Monday 8 January 2018

Simba Yatolewa Kombe la Mapinduzi Zanzibar

Mchezaji wa Simba, Moses Kisanzu (kulia) akiwania mpira na mchezaji wa URA, wakati wa mchezo wa Kombe la Mapinduzi uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar jana. Simba walilala kwa bao 1-0. 
Na Mwandishi Wetu
SIMBA ya Dar es Salam jana iliaga michuano Kombe la Mapinduzi baada ya kulambwa bao 1-0 na URA ya Uganda katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Kipigo hicho kimeifanya Simba kubaki na pointi zake nne, huku Waganda URA kufikisha pointi 10 na kutinga nusu fainali kwa kishindo.

URA imeifuata Azam FC nusu fainali kutoka katika kundi lao, huku kundi jingine Singida United na Yanga wakiwa tayari wamekata tiketi ya kucheza hatua hiyo.

Dakika 30 ya mchezo John Bocco nusura aifungie Simba lakini mpira wake aliupiga kwa kichwa ulipanguliwa na kipa wa URA, Aliozi Nafian nakuwa kona ambayo haikuzaa matunda.

Simba walikosa tena bao katika dakika ya 59 mfungaji akiwa Mosses Kitandu baada ya kupiga shuti kali lililokwenda nje ya goli.

Simba walikosa bap katika dakika ya 75 baada ya kutokea piga nikupige katika lango la wapinzani wao,lakini mabeki wa URA waliokoa kabla washambuliaji wa Simba hawajaleta madhara.

Vikosi vilikuwa URA, Alionzi Nafian, Kibunda Enock, Brian Majegwa, Allan Munaaba, Patrick Mbowa, Julius Mutyaba, Nicholas Kagaba, Deboss Kalama/Kulaba Jimmy, Peter Lwasa/Kamazi Denis, Mosses Sseruyide/Hudu Mulikyi na Shafiki Kagimo.


Simba: Emmaniel Mseja, Nicholas Gyan/Said Ndemla, Asante Kwasi, Juuko Murshid, Erasto Nyoni, Jonas mkude/Yusuf Mlipili, Mwinyi Kazimoto/James Kotei/, Mzamiru Yassin/Mavugo, Mosses Kitandu, John Bocco na Shiza Kichuya/Mohamed Ibrahim.

No comments:

Post a Comment