Tuesday 2 January 2018

Mama Ataka Mwanae Amlipe Gharama za Malezi

TAIPEI, Taiwan
MAHAKAMA Kuu nchini Taiwan imemuamuru mtu mmoja kumlipa mama yake karibu kiasi cha dola milioni 1 (sawa na pauni 710,000) kwa kumlea na kumsomesha udaktari wa meno.

Mama alisaini mkataba na mtoto wake mwaka 1997, wakati mtoto huyo akiwa na umri wa miaka 20, ukieleza kuwa atamlipa mama yake asilimi 60 ya kipato chake cha mwezi endapo atafaulu masomo hayo.

Mama alimburuza mwanae mahakamani baada ya kugoma kumlipa kwa miaka kadhaa kama walivyokubaliana katika mkataba.

Mtoto huyo alikuwa akidai kuwa ni kosa kwa mama yake kudai kurejeshewa gharama zake za matunzo ya mtoto huyo, lakini mahakama ilisisitiza kuwa mkataba huo uni halali na mtoto alitakiwa kumlipa mama yake.

Aliamriwa kumlipa mama huyo gharama zote pamoja na riba.

Mama huyo aliyejulikana kwa jina lake la ukoo la Luo, aliwalea watoto wake wote wawili yeye mwenyewe baada ya kuachana na mumewe miaka mingi iliyopita.

Bi Luo alisema alitumia maelfu ya dola kwa kuwatunza watoto wake hao wa kiume kwa kuwasomesha katika shule ya matibabu ya meno, lakini mama huyo alikuwa na wasiwasi kuwa hawatakuwa tayari kumlea wakati wa uzee wake.

Mama huyo alisaini mkataba na watoto wake hao wote wawili wakikubaliana kuwa watamlipa sehemu ya mapato yao kama malipo kwa ada ya shule, hadi kiasi cha dola za Marekani milioni 1.7.

Mtoto mkubwa alifikia makubaliano na mama yake na kuweka mkataba kwa kiasi kidogo, vyombo vya habari vya hapa vilieleza.

Hatahivyo, mtoto mdogo, aliyetambulika kwa jina mmoja la mwisho la Chu, alidai mahakamni hapo kuwa alikuwa mdogo wakati huo akisaini mkabata huo, na kutaka mkataba huo uchukuliwe kuwa haukuwa halali.

Bwana Chu pia alidai kuwa alifanya kazi kwa miaka kadha akatika kriniki ya meno ya mama yake baada ya kuhitimu na alimsaidia mama huyo kutengeneza fedha zaidi kuliko kiasi alichotakiwa kumlipa.

Msemaji wa Mahakama Kuu alisema majaji walikubaliana kuwa mkataba huo ulikuwa halali kwani uliingiwa wakati mtoto huyo tayari alikuwa mtu mzima na hakulazimishwa kufanya hivyo.


Chini ya vifungu vya sheria vya Taiwani, watoto wakiwa watu wazima wanalazimika kuwahudumia wazazi wao wanapozeeka.

No comments:

Post a Comment