Thursday 4 January 2018

Simba Yafanya Maangamizi Kombe la Mapinduzi

Na Mwandishi Wetu
SIMBA Sports Club usiku wa kuakia leo imetoka na pointi tatu muhimu baada ya kuifunga Jamhuri ya Pemba katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar kwa mabao 3-1.

Huo ni ushidi wake wa kwanza katika michuano hiyo baada ya kulazimishwa ya kufungana bao 1-1 na Mwenge katika mchezo wa Kundi A.

Simba tangu mwanzo wa mchezo huo ilionekana kuwa moto wa kuotea mbali baada ya kuwa mbele kwa mabao 2-0 hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, kwa mabao ya washambuliaji wake, John Raphael Bocco na chipukizi Moses Kitandu.

Kipindi cha pili, Simba iliendelea kutawala mchezo na kufanikiwa kupata bao la tatu lililofungwa na mchezaji mpya, beki Mghana, Asante Kwasi aliyesajiliwa kutoka Lipuli ya Iringa katika dakika ya 58.

Jamhuri wakafanikiwa kupata bao la kufutia machozi dakika tatu kabla mchezo huo haujamalizika likiwekwa kimiani na mshambuliaji wao, Moses Nassro.

Baada ya mchezo hyo, jopo la Makocha limemchagua mchezaji wa Simba kiungo Mwinyi Kazimoto kuwa mchezaji bora wa mchezo huo.

Kikosi cha Jamhuri kilikuwa; Ali Suleiman Mrisho, Mohammed Mwalimu, Mohammd Said, Mohammed Juma, Yussuf Makame Juma, Greyson Gerard Gwalala, Mussa Ali Mbarouk, Abdulatif Omar Mbarouk, Khamis Abrahman Ahmad, Mwalimu Mohammed Khalfan na Ahmed Ali Omar.


Simba Sports Club; Emmanuel Mseja, Erasto Nyoni, Shiza Nyoni, Juuko Murshid, Asante Kwasi, James Kotei, Nicholas Gyan, Muzamil Yassin, Moses Kitandu, John Bocco na Mwinyi Kazimoto.

No comments:

Post a Comment