Monday 1 January 2018

Diego Coasta atambulishwa rasmi Atletico Madrid

MADRID, Hispania
MSHAMBULIAJI wazamani wa Chelsea Diego Costa (pichani) ametambulishwa rasmi katika klabu ya Atletico Madrid na huenda akaanza kuichezea klabu hiyo wiki hii.

Costa ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Hispania alikubali kusaini mkataba na klabu hiyo ya La Liga Septemba lakini hakuweza kucheza kutokana na klabu hiyo kufungiwa kusajili.

"Nilikuwa nikiisubiri kwa muda mrefu siku hii, nilikuwa nikijaribu kufanya mazoezi na sasa ninahitaji kucheza, “alisema Costa juzi.

Atletico itacheza dhidi ya Lleida Esportiu kesho katika mchezo wa Kombe la Mfalme.

Costa juzi alitambulishwa rasmi katika klabu hiyo katika hafla iliyofanyika kwenye Uwanja wa Wanda, pamoja na Mhispania mwenzake Vitolo, aliyesaini katika timu hiyo akitokea Sevilla Julai.

Baadae alifanya mazoezi ya wazi, ambako vyombo vya habari vya hapa viliwakilishwa na waandishi 20,000.

"Nimekuwa nikifanya kazi kwa bidii na kujifua kwa nguvu lakini sikuwa na kitu kingine cha kufanya, “alisema Costa.

"Niko katika kiwango kizuri sana zaidi ya nilivyowasili hapa, nimejiandaa vizuri na kufanya kazi kwa bidii na kwa sasa niko tayari kwa kucheza na kuisaidia timu yangu kufunga mabao.”

Atletico Madrid ilikuwa katika kifungo chakusajili kwa vipindi viwili vya madirisha ya usajili baada ya kuvunja sheria ya usajili wachezaji wakigeni wenye umri chini ya miaka 18.

Lakini kifungo hicho kimemalizika jana Januari mosi na hiyo ina maana kuwa Costa anaweza kuanzakuichezea timu hiyo kesho, huku mchezo wake wa kwanza wa ligi ukiwa Jumamosi nyumbani dhidi ya Getafe.
Costa, ambaye aliondoka Atletico nakujiunga na Chelsea mwaka 2014, alifunga mabao 59 katika mechi 120 alizoichezea the Blues.


Alirejea Atletico, ambayo iko katika nafasi ya pili ya La Liga lakini iko pointi tisa nyuma ya vinara Barcelona, ikiwa ni miaka mitatu na nusu tangu alipoondoka katika klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment