Tuesday 28 April 2015

Jeshi la Nigeria laokoa wasichana 200 na akina mama 93



Kundi la wasichana wa Nigeria waliotekwa na Boko Haram kutoka kijiji cha Chobok mwaka 2014. Bado haijathibitishwa kama wasichana hao waliookolewa ni wale kutoka Chibok.


LAGOS, Nigeria
JESHI la Nigeria limewakomboa wasichana 200 na akina mama 93 ambao walitekwa na kundi la kigaidi la Boko Haram.

Hilo lilitokea wakati wa zoezi la kijeshi kuurejesha msitu wa Sambisa uliopo kaskazini ya Nigeria kutoka kwa kundi la kijeshi la Kiislamu.

Hatahivyo, ilithibitishwa kuwa watu hao waliookolewa sio wale wasichana wakiwemo wanafunzi 300 Wakristo waliotekwa mwaka jana huko hibok na kundi hilo.

Jeshi liliweka katika ukurasa wao wa Twitter taarifa ikisema: 'Jeshi mchana huu iliwaokoa wasichana 200 na akina mama 93 kutoka msitu wa Sambisa. 

'Hatuwezi kuthibitisha kama wasichana wa Chibok wamo katika kundi hili la watu walookolewa,' ilisema taarifa hiyo, ikiongeza kuwa jeshi la Nigeria pia limeharibu kambi tatu zinazoendeshwa na askari hao wa Boko Haram.

Baada ya kutekwa na Boko Haram, baadhi ya wasichana walionekana katika picha wakiwa wamevalishwa mavazi marefu ya hijab.
Wanadiplomasia na wapigania haki za binadamu wamesema kuwa wanaamini kuwa wasichana hao walikuwa wakishikiliwa msituni umbali wa karibu maili 60 kutoka Chibok.

Jeshi la Nigeria likisaidiwa na ndege za kivita lilivamia msimu huo ambao ni eneo la zamani la msimu wa hifadhi la kikoloni mwishoni mwa wiki iliyopita ikiwa ni sehemu ya zoezi la kutaka kulipokonya jimbo hilo kutoka kwa Boko Haram.

Kanali Sani Usman alisema: 'Jeshi liliokoa wasichana 200 na wanawake 93.

'Hatahivyo, sio wale kutoka Chibok, kijiji ambacho zaidi ya wasichana 200 walitekwa Aprili mwaka 2014.

'Hadi sasa, (jeshi) limeharibu na kufagia kabisa Sassa, Tokumbere na kambi zingine mbili katika eneo la Alafa, zote zikiwa katika msitu wa Sambisa.

Taarifa hiyo ilisema kuwa wasichana na akina mama hao watafanyiwa vipimo vya afya ili kujua kama walitekwa nyara au kuolewa na askari hao wa Boko Haramu.

'Kesho pia watahojiwa kujua kama walikuwa ni wake wa askari wa Boko Haram, kama wanatoka Chibok, au wako kwa muda gani katika kambi, na kama wana watoto.

Boko Haram waliteka wanafunzi wakike 200 karibu na kijiji cha Chibok Aprili mwaka jana, ambapo jumuiya ya kimataifa imelaani kitendo hicho.

Wanafunzi hao walichukuliwa katika malori usiku wa Aprili ya tarehe 14 na 15, abaada ya magaidi kutoka Boko Haram-wakidai kuwa elimu ya Magharibu ni dhambi-na walivunja shule kwa kujidai kuwa wao ni walinzi.

Wanafunzi hao walilazimishwa kubadili dini na kuwa Waislamu na kuolewa na wanajeshi wa kundi hilo.

Dunia nzima ililaani uvamizi huo na kufanya kampeni kubwa inayojulikana kama '#bringbackourgirls' lakini zaidi ya 200 bado hawajapatikana huku wengine wakidhaniwa kuwa waliachiwa au kuuawa.

Wiki iliyopi Nigeria niliadhimisha mwaka mmoja tangu kupotea kwa wasichana hao huku rais mpya wan chi hiyo Muhammadu Buhari, aliyeshinda uchaguzi wa urais wiki mbili zilizopita, alisema kuwa watafanya kila njia kuhakikisha wasichana hao wanarejeshwa nyumbani.

'Serikali yangu itafanya kila iwezalo kuwarejesha nyumbani wasichana hao, aliongeza rais huyo.

No comments:

Post a Comment