Monday, 6 April 2015

Emenike na wenzake washtushwa basi kushambuliwaISTANBUL, Uturuki
MSHAMBULIAJI wa Nigeria Emmanuel Emenike anasema yeye na wachezaji wenzake wa Fenerbahce waliachwa na mshituko baada ya basi la timu yao kushambuliwa kwa risasi Jumamosi usiku huko Uturuki.

Vinara hao wa Ligi Kuu ya Uturuki walikuwa wakisafiri kwenda uwanja wa ndege wa Trabzon ili kuapanda ndege na kurejea Istanbul, kufuatia ushindi wa bao 5-1 dhidi ya Rizespor, wakati shambulio hilo lilipofanyika.

Dereva wa basi hilo alikimbizwa hospitalini baada ya kujeruhiwa wakati wa shambulizi hilo, ambalo Emenike alilielezea kama tukio la kutisha ".

    Namtakia dereva wetu kila la kheri apone mapema. Wakati wote tunamtakiwa mema na askari wetu kwasababu basi lingeweza kutumbukia darajani”.

No comments:

Post a Comment