Friday 24 April 2015

Simba hatarini kuikosa hata nafasi ya pili



 *Yaiombea Azam ifungwe na Stand United na wao waichape Ndanda


Kikosi cha Simba.
Na Mwandishi Wetu
LIGI Kuu Tanzania Bara imefikia patamu wakati Yanga ikibakisha pointi tatu tu kutangaza ubingwa, vita kali inayoendelea ni ile ya kuwania kuwania nafasi ya pili kati ya mabingwa watetezi Azam FC pamoja na Simba.

Azam FC leo wanacheza na Stand United ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi Mbagala wakati Simba leo watakuwa wenyeji wa Ndanda FC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Simba inayoshuka dimbani leo,  endapo itafungwa na Ndanda FC ya Mtwara na Azam FC ikiifunga Stand United, basi wekundu hao wa Msimbazi watakuwa wameondolewa katika mbio hizo za kusaka nafasi ya pili.

Simba ikifungwa leo itakuwa na uwezo wa kufikisha pointi 44 huku Azam FC endapo itashinda leo itakuwa imefikisha pointi 45, ambazo hata kwa dawa haziwezi kufikiwa na wekundu hao wa Msimbazi.

Simba wenyewe kwa sasa wanasaka nafasi ya pili ili kupata kuliwakilisha nchi katika mashindano ya Kombe la Shirikisho la Afrika.

Kimsimamo kabla ya mchezo wa leo, Azam imecheza mechi 22 na hivyo kubakisha nne na ikishinda zote itaweza kufikisha pointi 54, ambazo Yanga itazipita endapo itashinda mchezo wake wa Jumatatu dhidi ya Polisi Moro kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Azam leo ikishinda itafikisha pointi 45 na itabakisha pointi tatu ili kufikisha 48 na kuiweka kando kabisa Simba katika mbio hizo za kusaka nafasi ya pili, kwani uwezo wa Simba ikishinda mechi zote, itafikisha jumla ya pointi 47 tu.

Aidha, Mbeya City itawakaribisha  Kagera Sugar katika mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa  Sokoine jijini Mbeya.

Simba inahitaji kushinda mchezo huo kama kweli inahitaji kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, lakini bado ina changamoto kama Azam watashinda kwani nao pia wanatafuta ushindi ili kugombania taji au kuendelea kubaki katika nafasi hiyo.

Simba na Azam Fc zinatofautiana kwa pointi nne, mmoja akishinda na mwingine akashindwa kuna atakayeshuka na mwingine kupanda kwa vile tofauti ya pointi itakuwa ndogo hivyo, kila timu inahitaji ushindi kuhakikisha inaendelea kutetea nafasi ilizonazo.

Timu ya Ndanda FC ambao katika mchezo wa raundi ya kwanza walifungwa na Simba mabao 2-0 uliochezwa Nangwanda Sijaona, wako katika hali mbaya, kwani wanashika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 25.

Iwapo watashindwa kuonyesha juhudi katika mchezo huo watazidi kuwa hatarini kwasababu tayari wameshacheza michezo 23 na wamebakiza mitatu kuanzia wa leo hivyo ushindi ni muhimu kwao.

Mabingwa watetezi Azam FC licha ya kujifariji kuwa wana nafasi ya kutetea ubingwa wao, pia wanahitaji kuonyesha juhudi kwa vitendo ili kufanya vizuri.

Kikosi cha Azam FC.
Azam FC wamekuwa wakisuasua katika baadhi ya mechi zao zilizopita na hivyo kuachwa kwa pointi na vinara wa ligi Yanga.

Timu wanayokutana nayo Stand United licha ya Azam kuwafunga raundi ya kwanza bao 1-0 huwa hawatabiriki, kwani Azam ikizembea Stand inaweza kuwatoa nishai.

Kwa upande wa Mbeya City na Kagera Sugar zimetofautiana kwa tofauti ya pointi tatu hivyo kila mmoja ni muhimu kushinda.

Kagera Sugar kama itashindwa kufanya vizuri kuna hatari ya kushuka kwani timu tano zilizoko  nyuma yake ikiwemo hiyo ya Mbeya City zinafanana kwa pointi 28, kwa maana kwamba zote zikifanya vizuri inaweza kujikuta ikiangukia nafasi ya 10.

Michezo mingine itakayopigwa kesho Jumapili ni Mtibwa Sugar wakicheza dhidi ya JKT Ruvu kwenye uwanja wa Manungu na Tanzania Prisons wakiwakaribisha Mgambo JKT kwenye uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.

Msimamo:




MP
W
D
L
GF
GA
+/-
Pts


1

23
16
4
3
47
14
33
52


2

22
11
9
2
29
15
14
42


3

23
10
8
5
31
17
14
38


4

23
8
7
8
22
22
0
31


5

24
7
8
9
16
26
-10
29


6

23
6
10
7
22
23
-1
28


7

23
6
10
7
19
21
-2
28


8

23
7
7
9
21
27
-6
28


9

23
8
4
11
18
25
-7
28


10

24
6
10
8
16
23
-7
28


11

23
6
7
10
17
23
-6
25


12

24
5
10
9
15
22
-7
25


13

23
6
7
10
18
26
-8
25


14

23
3
13
7
15
22
-7
22

No comments:

Post a Comment