Tuesday, 5 May 2015

Mahakama Burundi yamruhusu Pierre Nkurunziza kugombea uraisBUJUMBURA, Burundi
MAHAKAMA ya Kikatiba nchini Burundi imemruhusu rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu wa urais katika uchaguzi uliopangwa kufanyika baadae mwaka huu.

Kulingana na vituo vya redio nchini humo,Jaji wa mahakama hiyo alitoa uamuzi huo mapema leo asubuhi na kumruhusu rais huyo kuwania tena urais pamoja na vurugu zilizopo.

Jana jaji msaidizi wa mahakama hiyo Jaji Sylvere Nimpagaritse, alilitoroka taifa hilo akidai kuwa walikuwa wakishinikizwa kutoa uamuzi utakaompendelea rais Nkurunziza.

Rwanda imethibitisha kuwa jaji huyo yuko mjini Kigali nchini Rwanda ambako ametafuta hifadhi.

No comments:

Post a Comment