Friday, 3 April 2015

Kell Brook achukizwa na dharau za Khan
LONDON, England
BINGWA wa dunia wa uzito wa welter Kell Brook (pichani), amemkosoa mpinzani wake Mwingereza Amir Khan kwa kuonesha "dharau ".

Brook, mwenye umri wa miaka 28, Jumamosi alitwaa tena taji la IBF na alitaka kupigana na Khan, ambaye pia ana miaka 28, ambaye aliamua pambano lake lijalo liwe dhidi ya Mmarekani Chris Algieri.

Awali, Khan alikubali pambano lake lijalo liwe dhidi ya Brool, lakini baadae alibadili na kutaka kupigana na Mmarekani.

"Khan hameoesha dharau kwangu na alikuwa akiangalia chini, lakini nimefanya kila kitu…, " alisema Brook.

"Mimi ni bondia ambaye sijapigwa na ninastahili kupewa heshima lakini alizungumza na mimi kama sina kitu."

Khan, bingwa wazamani wa dunia katika uzito wa light-welter, alielezea nia yake ya kupigana na Floyd Mayweather au Manny Pacquiao huko mbeleni, lakini alisema huenda akapigana na Brook "ndani ya miezi 12 ijayo ".

Hatahivyo, Brook ambaye maskani yake huko Sheffie ameshinda mapambano yake yote 34 ya kulipwa, alielezea kushangazwa na chaguao la Khan la kutaka kupigana na Algieri kama mpinzani wake ajaye.

No comments:

Post a Comment