Thursday, 16 April 2015

Somalia kurejea fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2019MOGADISHU, Somalia
RAIS wa Chama cha Soka cha Somalia Adbi Qani anatumaini nchi yake itashindana katika fainali za Mataifa ya Afrika za mwaka 2019 na kumaliza kutoshiriki tangu mwaka 1974
 .
Nchi hiyo ilishiriki mara moja tu fainali hizo za Mataifa ya Afrika, kutokana na matatizo ya kisiasa, kutokuwa na pesa na tatizo kubwa la miundo mbinu.

Na nchi hiyo pamoja na majirani zao Eritrea ndio nchi pekee wanachama wa Shirikisho la Soka la Afrika (Ca0, ambazo hazitashiriki katika fainali za mwaka 2017 kati ya mataifa 54 wanachama.

Lakini Qani anaamini kuwa kwa kumalizika ujenzi wa uwanja mpya ambao ujenzi wake unatarajia kukamilk==ika baadae mwaka huu, nchi hiyo itakuwa tarajia kurejea tena katika michuano hiyo kabla ya kumalizika kwa muongo huu.

No comments:

Post a Comment