Thursday, 2 April 2015

TUME YA UCHAGUZI: KURA YA MAONI KUTOFANYIKA APRILI 30 
Na Mwandishi Wetu
TUME ya Uchaguzi (NEC) imesema haitoweza kuendelea na zoezi la kura ya maoni kama ilivyopangwa kufanyika Aprili 30, kutokana na kutokamilika kwa zoezi la uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura.

Akiongea leo Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Damian Lubuva (pichani) amesema kuwa zoezi lolote la kupiga kura likiwepo la kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa linategemea kuwepo kwanza kwa daftari la kudumu la wapigakura.

Licha ya kutangaza kuhairishwa zoezi la upigaji kura ya maoni hadi baadae, Jaji Lubuva amesema zoezi la uboreshwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura litaendelea katika mikoa ya Lindi, Ruvuma, Iringa na Mtwara.No comments:

Post a Comment