Thursday, 9 April 2015

Maambukizi yaliyotokana na brashi ya `makeup' yamfanya kupooza kabisaCANBERRA, Australia
MAMA mmoja nchini Australia amekuwa akipambana ili kupona maambukizo ya ngozi, ambayo yanatishia maisha yake na kumuacha akiwa nusu amepooza.

Tatizo hilo alilipata baada ya kuazima brashi ya `makeup.
Gazeti la The Daily Mail la Australia liliripoti kuwa Jo Gilchrist Siku ya Wapendao ndio alianza kujisikia maumivu katika mgongo wake na baadae maumivu hayo yaliongezeka na kujisikia vibaya zaidi ya maumivu anayopata mama wakati wa kujifungua.

Baadae mdada huyo alianza kupoteza hisia katika miguu yake na sehemu ya chini ya mwishi na kukimbizwa hospitali kwa kutumia ndege hadi Brisbane kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa dharura.

Inaelezwa kuwa maambukizi hayo yalipatikana baada ya kutumia brashi ya kujipambia ya rafiki yake kwa ajili ya kuziba chunisi usoni.
 
Jo Gilchrist, 27, aliachwa amepooza kutokana na maambukizo hayo ya ngozi aliyoyapata kutoka katika brashi ya rafiki yake ya kujipambia.

“Rafiki yangu alikuwa na maambukizo usoni mwake na mimi nilitumia brashi yake” alisema dada huyo. Sikujua kama hilo litatokea. Nilikuwa naazima brashi za wenzangu mara kwa mara.

Maambukizo hayo yameharibu kabisa uti wa mgongo, na madaktari walisema kuwa dada huyo hatatembea tena. Lakini Gilchrist, 27, amekuwa akifanya kazi kuthibitisha kuwa madaktari hawakuwa sahihi, na ameenda kufanya mazoezi ili kujaribu kuponya miguu yake.

"Ni hali ngumu ambayo sijawahi kukutana nayo," aliandika katika ukurasa wake wa Facebook. "Nimekuwa nikilala sana usiku na mchana na kupata maumivu kibao.

Matibabu ya nguvu kupitia mazoezi yamemsaidia kuanza kusogeza miguu yake taratibu, kusimama na kupiga hatua chache wakati wa mazoezi hayo.

No comments:

Post a Comment