Sunday, 12 April 2015

Mwanamke wa Misri avaa kiume miaka 40 ili kupata chakula cha familia yake
Mwanamke wa Misri Sisa Abu Daooh (kushoto), akipokea tuzo kutoka kwa rais wa nchi hiyo, Abdel-Fattah El-Sissi.
CAIRO, Misri
KWA zaidi ya miongo minne (miaka 40), mama wa Misri Sisa Abu Daooh amekuwa akivaa kama mwanaume ili kumuwezesha kupata ajira kwa ajili ya kupata fedha za kuendeshea familia yake.

Mama huyo wiki iliyopita alizawadiwa tuzo ya "woman breadwinner" na serikali huko kwao Luxor na kupongezwa na rais wa Misri.

Abu Daooh, 65, wiki iliyopita alikuwa katika sherehe iliyofanyika katika makazi ya rais, ambako alikutana na Rais Abdel-Fattah El-Sissi na kupokea zawadi ya fedha ya kiasi cha dola za Marekani 6,500.

Akiwa amevalia joho la kiasili la kiume na kilemba wakati akipokea tuzo hiyo, ambapo alipongezwa na rais kama "mwanamke mfanyakazi asiyewakawaida.

Abu Daooh alikuwa na ujazito na mtoto wakike Houda wakati mume wake alipofariki dunia katika miaka ya 1970, akimuacha ndiye mtunzaji wa familia.

Abu Daooh alibaini haraka kuwa katika tamaduni za jamii ya Kimisri wakati huo, kulikuwa na nafasi chache sana za kufanya kazi kwa wanawake wasio na elimu kama yeye, na alikuwa rahisi kupata kazi ukiwa umevaa kama mwanaume.

Mama huyo baada ya kuvaa kama mwanaume alipata kazi katika sehemu ya kutengenezea matofali na kungarisha viatu, na aliamua kuvaa hivyo ili kukwepa kunyanyapaliwa.


"Ili kujilinda mwenyewe nisinyanyaswe na wanaume na kusakamwa kutokana na tamaduni zetuniliamua kuvaa kama mwanaume na kufanya kazi pamoja nao katika kijiji kingine ambako hakuna aliyekuwa akinijua, aliuambia mtandao huo.


Abu Daooh akibrash viatu huku akiwa amevaa vazi la kiume.
Hadi sasa, Abu Daooh bado anfanyakazi mbali na nyumbani kwao. Mume wa mtoto wakike wa Abu Daooh hawei kufanyakazi, hivyo mama huyo anaendelea kutafuta kipato kwa ajili ya familia yake.
“Mama yangu ni mmoja ambaye anaihudumia familia, " alisema mtoto wakike wa Abu Dooah.
"Kila siku anaamka saa 12 asubuhi na kuanza kungarisha viatu huko Luxor. Nambebea vitu vya kufanyia kazi kwa sababu sasa ni mtu mzima.
Abu Dooah alisema mama amekuwa akivaa nguo za kiume, na amesisitiza katika kipindi kilichobaki cha maisha yake ataendelea kuvaa nguo hizo. “Nimeamua kufaa katika nguo hizi. Katika maisha yangu yaliyobaki nitavaa nguo hizi, ” aliliambia gazeti moja.
No comments:

Post a Comment