Thursday, 2 April 2015

BFT yateua 17 kuunda timu ya taifa ya ndondi
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKISHO la Ndondi Tanzania (BFT) limeteua mabondia 17 watakaoingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya Michezo ya Afrika na mingine ya kimataifa, imeelezwa.

Katibu Mkuu wa BFT Makore Mashaga amesema kuwa, mabondia hao waliteuliwa katika mashindano ya kimataifa yaliyomazika hivi karibuni kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa na kushirikisha na mabondia wa Kenya na Uganda.

Alisema kuwa mashindano hayo yaliyofanyika Uwanja wa Ndani, yalikuwa na mafanikio makubwa na yalimaliziaka Jumamosi.

Mabondia waliochaguliwa kwa sasa taratibu za kuombewa ruhusa katika timu zao zinafanyika na taratibu hizo zitakapo kamilika watatakiwa kuanza mazoezi kabla ya tarehe 15.04.2015, kwa ajili ya kushiliki mashindano mbalimbali ya kitaifa.

Michezo ya Afrika itafanyika Brazzavile, Kongo kuanzia Septemba 4-19, mashindano ya ubingwa wa dunia ya Aiba Oktoba 5-18 Doha Qatar.

Mabondia waliochaguliwa kwa uzito wao ni kama ifuatavyo:-

49 kgs L/FLY
   Mohamed Mzeru JKT
   Maulid Athumani-
   Ibrahim Abdalah Magereza.

52 Kgs Fly Weight.
   Juma Ramadhani- Temeke
   Said Hofu- JKT

56 Kgs Bantam Weight
   Ahamad Furahisha- JKT
   Bon Mlingwa- JKT

60 Kgs Light weight.
   Elias Mkomwa- JKT
   Bosco Bakari- JKT
   Fabian Gaudence- NGOME

64 Kgs Light Weight

   Kassim Mbwitike- JKT

69 Kgs. Welter Weight.
   Said Gulushad JKT
   Seleman Bamtulah- JKT

75 Kgs Middle Weight.
   Ivan Mussa Kagera

81 Kgs light Heavy
   Hamidu Halfan-JKT

91 Kgs Heavy weight
   Alex Sitta- JKT
   Nuru Ibrahim- Magereza

Aidha,  BFT  inawapongeza mabondia wote kwa jitihada kubwa walizofanya na hatimae kuchaguliwa kuwa mabondia wa timu ya taifa ya ngumi 2015.

No comments:

Post a Comment