Tuesday, 7 April 2015

Yanga kuionesha Coastal makali ya CAF leo *Azama FC nao kibaruani Chamazi na Mbeya City

Na Mwandishi Wetu
YANGA mbayo imefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Afrika, leo itaionesha Coastal Union makali yake wakati timu hizo zitakapokwaana kwenye Uwanja wa Taifa katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Wawakilishi hao pekee wa Tanzania katika mashindano ya kimataifa, ndio viongozi wa ligi hiyo inayoshirikisha jumla ya timu 14 huku Azam FC ikishikilia nafasi ya pili katika msimamo.

Azam FC nao pia watashuka dimbani Chamazi Mbagala jijini Dar es Salaam abako watacheza na Mbeya City ya Mbeya katika mchezo unaotarajiwa kuwa mkali na wakusisimua.


Kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Yanga itawakaribisha Coastal Union ya Tanga, huku Azam FC ikiwa mwenyeji wa Mbeya City kwenye uwanja wao wa Chamazi, Mbagala.

Yanga  wana  pointi 40 wakiwa tayari wameshacheza michezo 19 na kubakiza saba, wakati Azam wana pointi 36 wakiwa wameshacheza michezo 18 na kubakiza minane, wakitofautiana na vinara hao kwa tofauti ya pointi nne.

Kama Yanga ili waendelee kuwa vinara wa ligi hiyo, wanahitaji kushinda mchezo wa leo. Halikadhalika, kwa Coastal Union ambao wanazidi kushuka siku hadi siku wanahitaji kushinda ili kujiepusha katika harakati za kushuka daraja.

Coastal Union ina pointi 24 ikiwa katika nafasi ya saba. Awali wakati wanaanza michuano ya ligi walikuwa wakienda vizuri lakini walianza kupoteza mwelekeo baadaye na kujikuta wakishuka kutoka nafasi ya tano hadi hiyo.

Timu hiyo ya Tanga imekuwa haitishi kama zamani, kwani sasa hupoteza michezo yake ya nyumbani tofauti na miaka iliyopita walikuwa wakiogopwa.

Katika mchezo wake wa hivi karibuni, ilikubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons.

Aidha, katika mchezo wa raundi ya kwanza dhidi ya Yanga, wagosi hao wa kaya walipokea kichapo cha bao 1-0, lakini huenda leo ikabadilika na kufanya vizuri ili kurejesha matumaini ya kufanya vizuri katika mechi za mwisho za ligi hiyo.

Hata hivyo, Yanga leo wanacheza na Coastal Union ikiwa chini ya kocha Jamhuri Kihwelo anayeinoa timu hiyo kwa muda kumalizia mechi zilizobaki za Ligi Kuu.

Kwa upande wa Mbeya City inayokutana na Azam FC, timu hiyo itakuwa na wakati mgumu kama itapoteza kwani inashika nafasi ya nane ikiwa na pointi 24.

Pointi ilizonazo timu hii ya Mbeya hazitoshi kuihakikishia kukwepa janga la kushuka daraja na hivyo inahitaji pointi zote tatu ili angalau kujihakikishia usalama.

Na Azam pia wanahitaji kushinda kwani nafasi yake itakuwa ngumu kama watapoteza kwa vile kuna uwezekano wa kushuka kutokana na kutofautiana kwa pointi moja na Simba, ingawa bado wana mechi nyingi kuliko Simba.

Katika mchezo  uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita,  Mbeya City ilitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Ndanda FC wakati Azam FC katika mchezo wake wa mwisho wa ligi walishinda 1-0 dhidi ya Coastal Union mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Timu zote zimekuwa zikitamba kuondoka na ushindi katika mchezo wa leo, na kila moja ikionyesha shauku ya kupambana ili kupata matokeo mazuri.


Msimamo:
PWDLGFGA+/-Pts

1
Young Africans19124328111740

2
Azam18106225121336

3
Simba SC2198427151235

4
Kagera Sugar217771920-128

5
Mgambo JKT208391719-227

6
Ruvu Shooting216871418-426

7
Coastal Union215971415-124

8
Mbeya City205961517-224

9
JKT Ruvu216691620-424

10
Ndanda216691824-624

11
Stand United206681723-624

12
Mtibwa Sugar205871921-223

13
Polisi Morogoro214981321-821

14
Tanzania Prisons2031161420-620


No comments:

Post a Comment