Monday 6 April 2015

Rodgers maji ya shingo kuwashawishi wachezaji kubaki




LONDON, England
KOCHA wa Liverpool Brendan Rodgers tayari anakabiliana na kibarua kigumu kumshawishi nyota Raheem Sterling kusaijili mkataba mpya wa kuendelea kuichezea timu hiyo.

Lakini gazeti la Starsport  lilibainisha kuwa kocha huyo pia ana kazi nyingine ya hatma ya Anfield kumshawishi kiungo Henderson naye kubaki katika klabu hiyo.

Henderson ametupilia mbali mkataba mpya ambao ungekuwa na thamani ya pauni 80,000 kwa wiki.
Mazungumzo zaidi yanafanywa lakini Chelsea wanafuatilia kwa makini sana suala hilo.
Macho yanamfuatilia zaidi Sterling hasa baada ya mchezaji huyo kupiga chini ofa ya Liverpool ya pauni Milioni 100,000 kwa wiki na kusimamisha mazungumzo yote hadi mwisho wa msimu.
Lakini Sterling bado amebakisha miaka miwili katika mkataba wake wasasa wakati makamu nahodha wa timu hiyo Henderson suala lake linaonekana ni nyeti zaidi wakati mkataba wake umebaki mwaka mmoja tu.

Muingereza Henderson sasa ni mchezaji muhimu kwa Liverpool, ambapo alinunuliwa na Liverpool kwa pauni Milioni 20 akitokea Sunderland mwaka  2011.

Matumaini ya Liverpool kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya yanazidi kufifia baada ya timu hiyo kushindwa kuwemo katika nne bora, kufuatia kichapo cha 4-1 Jumamosi dhidi ya Arsenal.

Na Rodgers anakiri kuwa, kutokuwemo katika Ligi ya Mabingwa huenda kukatupa wakati mgumu kusajili katika kipindi cha majira ya joto.

"Nafikiri wachezaji wengi wanataka kucheza katika mashindano makubwa na kama haupo katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya itakufanya wewe kuwa na wakati mgumu, " alisema.

Alipoulizwa kama matumaini ya kufuzu kwa Ligi Kuu ya Mabingwa wa Ulaya yamepotea, baada ya kufungwa na the Gunners na kufungwa nyumbani na Manchester United, Rodgers alisema: "Nafikiri hivyo.

No comments:

Post a Comment