Thursday, 16 April 2015

Kivumbi Ligi Kuu Tanzania Bara kutimka JumamosiKikosi cha Simba Sports Club.

Na Mwandishi Wetu
LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea tena Jumamosi kwa mechi kadhaa kuchezwa zikiwemo mbili zitakazovuta hisia za wengi za Simba na Mbeya City na Azam FC na Kagera Sugar.

 Simba iko katika nafasi ya tatu itakuwa mwenyeji wa Mbeya City iliyopo katika nafasi ya 10, ambayo msimu huu imekuwa ikifungika kirahisi tofauti na msimu uliopita, ambapo ilikuwa ikitoa vichapo hadi kwa vigogo.

Endapo Simba itashinda mchezo wake huo itakuwa imefikisha jumla ya pointi 38 huku ikiombea Azam FC ifungwe ili iendelee kubaki na pointi zake 39 baada ya Jumatano kutoka suluhu na Mgambo ya Tanga kwenye uwanja wa Mkwakwani.

Azam FC inakutana na Kagera Sugar yenye pointi 31 na iliyop katika nafasi ya nne katia mchezo utakofanyika kwenye uwanja wao wa Chamazi Mbagala jijini Dar es Salaam.

Mechi zingine hiyo Jumamosi ni kati ya Polisi Morogoro watakaocheza na Ndanda FC ya Mtwara kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro huku Stand United ya Shinyanga itakuwa na mtihani itakapocheza na JKT Ruvu.

Nayo Ruvu Shooting wataikaribisha Mgambo katika mchezo mwingine unaotarajia kuwa na msisimko wa aina yake kwenye uwanja wa Mabatini Mlandizi mkoani Pwani.

Polisi Morogoro ndio inayoshika mkia katika msimamo wa ligi hiyo inayoshirikisha jumla ya timu 14 huku Tanzania Prisons nayo ikiwa na pointi 21 sawa na Polisi Moro ikiwa katika nafasi ya pilikutoka mkiani.

 Msimamo
MP
W
D
L
GF
GA
+/-
Pts


1

21
14
4
3
39
12
27
46


2

21
10
9
2
27
14
13
39


3

21
9
8
4
27
15
12
35


4

22
8
7
7
21
20
1
31


5

21
8
4
9
17
19
-2
28


6

22
6
9
7
21
22
-1
27


7

21
7
6
8
18
23
-5
27


8

23
6
9
8
16
23
-7
27


9

22
6
8
8
14
20
-6
26


10

22
5
10
7
17
21
-4
25


11

22
6
7
9
18
24
-6
25


12

22
6
6
10
16
22
-6
24


13

22
3
12
7
14
21
-7
21


14

22
4
9
9
13
22
-9
21

No comments:

Post a Comment