Monday, 6 April 2015

Mourinho ataka Chelsea ishinde mechi sita tuLONDON, England
KOCHA Jose Mourinho (pichani), amewaambia wachezaji wa Chelsea kuwa, wanahitaji pointi 16 tu kutoka katika mechi zilizobaki ili kulikamata taji la Ligi Kuu ya England.

The Blues kwa sasa wako pointi saba mbele ya wapinzani wao wa karibu Arsenal na pointi na moja zaidi mbele ya Manchester United.

Kikosi hicho cha kocha huyo anayefahamika pia kama `the Special One’ , kina mchezo mmoja mkononi kabla hakijatimiza idadi sawa na timu zingine.

Kocha huyo Mreno, aliyerejea Stamford Bridge mwaka 2013, anaamini kuwa, timu yake inahitaji ushindi wa mechi tano zaidi na sare moja ili kuzifunika kabisa the Gunners na mashetani hao wekundu na kuiwezesha the Blues kutwaa taji lake la kwanza la ligi katika kipindi cha miaka mitano.

"Katika kipindi hiki, tunahitaji ushindi wa mechi tano na sare moja tu, " alisema Mourinho, ambaye anajulikana kwa ubwatukaji wake.

"Kila ushindi na sare ni hatua moja mbele. Wengi wanajua unatakiwa kushinda kila mchezo.

"Kwetu sisi, tunatakiwa kujifikiria wenyewe na kuwasahau wengine. Tunajua tuna mechi nane na tunahitaji ushindi wa mechi tano na sare moja tu, basi."

No comments:

Post a Comment