Thursday, 16 April 2015

Barcelona, Porto zatoa vipigo robo fainali Ulaya


Luis Suarez wa Barcelona (kulia) akimpiga tobo David Luiz wa PSG wakati akielekea kufunga bao lake la pili katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya juzi. Barca ilishinda 3-1.

PARIS, Ufaransa
TIMU za Barcelona na Porto juzi usiku zilianza vizuri mechi za kwanza za  robo fainali za Ligi ya Mabingwa wa Ulaya baada ya kushinda mechi zao.

Barcelona ilitoa kipigo cha bao 3-1 dhidi ya Paris Saint German (PSG) katika mchezo uliofanyika Ufaransa huku Porto ikiwalambisha sakafu mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich kwa idadi kama hiyo ua mabao.

Kutoka na kipigo hicho cha PSG, wadau mbalimbali wa soka wakiwemo makocha na wachambuzi wa soka walimlaumu vikali beki wa Bayern Munich Luiz wakidai kuwa makosa ya mlinzi huyo ndio yaliyoigharimu timu.

Beki huyo wazamani wa Chelsea aliingia akitokea benchi Jumatano katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya mashindano hayo na mara mbili alishindwa kuzuia wakati mabao mawili ya Luis Suarez yakitengenezwa.

Luiz aliumia siku 10 zilizopita lakini Hoddle, aliyesisitiza kuwa Mbrazil huyo mara nyingi huwa na uwezo wa kuzuia, anaamini bado alijitahidi pamoja na hakutokuwa fiti vya kutisha.

Alipoulizwa kuhusu uzuaiji wa Luiz wakati Barcelona ikifunga bao la tatu, mchambuzi huyo wa soka alisema: 'Hata kama hauko fiti kwa asilimia 100 huwezi kuonesha udhaifu wa namna ile.

'Yeye ni mtu wa mwisho uwanjani wakati Suarez akichukua mpira na kuanza kumkimbilia. Aligundua kuwa yeye ni mtu wa mwisho ukiwa mtu wa mwisho unachotakiwa kufanya kuruka. Unachelewesha ili wachezaji wenzake wafike.

'Lakini yeye alifanya kama mtoto wa miaka nane ambaye hajafundishwa mpira. Alijaribu kuuchukua mpira kwa kuingiza miguu yake yote miwili pamoja lakini alivyofanya hivyo alishindwa kusogea popote. Suarez alifanya vitu vyake tena.

Hatahivyo,mchambuzi mwenzake, ambaye ni mchezaji wazamani wa Arsenal Thierry Henry, haraka alimlaumu maelekezo ya kocha wa PSG  Blanc, ambaye aliamua kumuingiza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 baada ya kuumia kwa Thiago Silva.

Henry alisema: 'Ikiwa David Luiz haukuwa fiti vyakutosha kuanza mchezo, kwanini alimuingiza kama mchezaji wa akiba baada ya dakika 21?

'Kwa misingi ya ukocha, kwanini unamuingiza ikiwa hakuwa fiti vyakutosha?'

No comments:

Post a Comment