Wednesday 15 April 2015

Nyota kibao kushindana Ngorongoro Marathoni Jumamosi



 *Sumaye mgeni rasmi katika mbio za mwaka huu

Baadhi ya washiriki wa Ngorongoro Marathoni.
Na Mwandishi Wetu
WANARIADHA kibao nyota wamethibitisha kushindana katika mbio za Ngorongoro Marathoni, ambazo zitafanyika Jumamosi Aprili 18 zikishuhudiwa na Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Fredirick Sumaye.

Kwa mujibu wa mratibu wa wachezaji katika mbio hizo za kila mwaka, Sumaye ndiye atakayekuwa mgeni rasmi ambapo ataanzisha mbio hizo katika lango la kuingilia na kutokea katika mbuga na bonde la Ngorongoro.

Pia baada ya kuzianzisha mbio hizo ambazo mwaka huu zinatarajia kushirikisha zaidi ya wanariadha 500 kutoka ndani na nje ya nchi, Waziri Mkuu huyo wa awamu ya tatu ya uongozi nchini, atakabidhi zawadi kwa washindi kwenye uwanja wa Mazingira Bora mjini Karatu.

Mary Naali atashiriki mbio za mwaka huu.
Nyota Kibao Kushiriki:
Petro alisema kuwa miongoni mwa wanariadha waliothibitisha kushiriki mbio hizo ni pamoja na nyota waliounda timu ya taifa ya riadha iliyomaliza ya sita katika mashindano ya dunia ya mbio za nyika huko, ambao ni Bazil John, Ismail Juma, Joseph Panga, Alphonce Felix na Fabiano Sulle.

Mbali na hao pia bingwa wa mbio za Kilimanjaro Marathoni (kilometa 42) kwa upande wa wanawake mwaka huu Fabiola William, bingwa wa mbio za nyika za taifa Catherine Lange, mkali wa mbio kibao nchini Failuna Abdi na Nathaeli Elisante aliyeshika nafasi ya pili mwaka jana.

Kwa mujibu wa Petro wakali wengine watakaoshiriki mbio hizo ambazo kila mwaka zimekuwa zikikuwa kwa kasi kubwa chini ya Zara Tanzania ni pamoja na Fabian Joseph, Dickson Marwa, Pendo Japhet, Mary Naali na wengine wengi.

Dickson Marwa (kushoto) amethibitisha kushiriki mbio za mwaka huu.
Zawadi kwa Washindi:
Petro ambaye ni mwanariadha nyota wazamani wa Tanzania alisema kuwa washindi wote mwaka huu watapata zawadi sawa bila kujali jinsi zao, tofuat na mashindano mengi ambayo wanawake hupata zawadi kidogo ukulinganisha na wanawaume
.
Mshindi wa kwanza kwa wanawake na wanaume, kila mmoja ataondoka na kitita cha Sh. Milioni 1 wakati wa pili ataondoka na kiasi cha Sh. 500,000 na watatu ni 250,000.

Alisema kuwa mashindano ya mwaka huu yanafanyika chini ya udhamini wa Zara Tanzania, Bonite, African Safari, Exim Bank, CRDB Bank, Marenga Investment, Africa Safari, Hans Park,Red & White Wine.

Mtoto akivishwa medali baada ya kushinda mbio za kilometa 2.5.
Lengo la Mbio Hizo:
Awali, lengo kuu la kuendesha mbio hizo ambazo mwaka huu zinakimbiwa kwa mara ya nane, lilikuwa ni kupiga vita ugonjwa wa malaria katika jamii za wamasai.

Hatahivyo, baada ya lengo hilo kufanikiwa na ugonjwa huo kupungua, mwaka huu lengo ni kuwaisaidia jamii hiyo katika tatizo la elimu na afya ikiwemo ile ya uzazi.
Lazaro Nyarandu; Waziri wa Maliasili na Utalii akisalimiana na mmoja wa waratibu wa mbio hizo huku rais wa Riadha Tanzania (RT) (kushoto) Anthony Mtaka akishuhudia.

No comments:

Post a Comment