Sunday 26 April 2015

Tetemeko la ardhi laua watu 3,000 Nepal




KATHMANDU, Nepal
ANGALAU watu 3,218 sasa wanafahamika kuwa wamekufa kutokana na tetemeko kubwa la ardhi lililotokea nchi Nepal Jumamosi, imeelezwa.

Kiongozi wa wakala wa majanga na maafa wa Nepal, Rameshwor Dangal alisema kuwa watu wengine 6,500 wamejeruhiwa kutokana na madhara yaliyotokana na tetemeko hilo la ardhi.
Pia watu kibao wameripotiwa kuuawa katika nchi za jirani za China na India.

Maelfu ya watu walitumia usiku wa pili nje baada ya tetemeko lenye ukumbwa na magnitude 7.8, ambalo pia liliua katika mlima wa Everest lilitokea.

Taarifa zinasema kuwa vikosi vya uokoaji nchini humo vimezidi kuimarishwa baada ya kutokea kwa tetemeko hilo.

Kwa mujibu wa maofisa nchini humo, tetemeko hilo ni kubwa na limesababisha madhara makubwa, ambayo hayajawahi kutokea kwa muda wa miaka 80 sasa.

Tayari nchi nyingi na mashirika ya misaada yamejitokeza kusaidia wale wote walioathirika na tukio hilo lililochukua uhai watu na kuharibu majengo na mali zingine.

Zaidi ya watu 17 walipoteza maisha katika Mlima Everest baada ya kuanguka kwa theluji.

Theluji hiyo pia ilisababisha maafa katika maeneo mengine jirani na Nepal kama India na Bangladesh.

Tetemeko lenye ukubwa wa magnitude 6.7 lilisikika Mashariki mwa Nepal katika Jiji la Kathmandu na kusababisha taharuki baada ya watu kuanza kukimbia bila mpangilio.

Kutokana na tetemeko hilo,theluji katika mlima huo wa Everest lilianza kuanguka na kusababisha madhara hayo katika maeneo tofauti tofauti yanayouzunguka mlima huo.

Baada ya tetemeko hilo kubwa muda mfu;I baadae lilifuatia tetemeko lingine lenye ukubwa wa magnitude 6.6. Jumapili asubuhi lilitokea jingine Nepal lenye ukumbwa na magnitude 6.7.

Taarifa zaidi kutoka nchini humo ziliongeza kuwa, idadi ya watu waliokufa kutokana na tetemeko hilo, imeongezeka baada ya maeneo mengi ya vijijini kushindikana kupatikana kwa taarifa kamili za vifo na majeruhi.

Pamoja na vifo na uharibifu huo mkubwa wa vitu na mali, matetemeko hayo yamesababisha kukatika kwa mawasiliano nchini humo, zikiwemo barabara kukatika na milima kuporomoka.

Zaidi ya watu 700 wamepoteza maisha jijini Kathmandu pekee, huku miili mingi ikisafirishwa kwa boti na kuhifadhiwa katika hospitali mbalimbali jijini humo.
 

No comments:

Post a Comment