Sunday 23 October 2016

Man United wachezea kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa Chelsea, Man City ikilazimishwa sare ya 1-1



LONDON, England
TIMU ya Chelsea leo imefanya kweli baada ya kuutumia vizuri Uwanja wao wa nyumbani baada ya kuikandamiza Manchester United kwa mabao 4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.

Chelsea imemuumbua kocha wao waamani Jose Mourinho ambaye kwa sasa anayeinoa Manchester United ambayo pia inashiriki katika michuano ta lii ndoo ya Ulaya.

Katika mchezo huo unaoelekekea ukinoni kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, mabao ya wenyeji Chelsea yaliwekwa kimiani na  Pedro katika dakika ya kwanza wakati bao la pili liliwekwa nyavuni na Cahill katika dakika ya 21 huku Hazard akicheka na nyavu katika dakika ya 70 Kante akifuna katika dakika ya 70 na na 75.

Katika mchezo uliotanulia, Manchester City imerejea kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu ya England licha ya kuepata sare ya tano dhidi ya Southampton na kuondoka na pointi moja.

Wageni ndio walikuwa wa kwanza kupata bao ambalo lilipatikana baada ya pasi ya John Stones kumuwezesha Nathan Redmond kumzunuka Claudio Bravo na kufunga bao lililojaa wavuni.

City waliimarika baada ya awali kuzomewa na mashabiki pale walipopata bao la kusawazisha lililofungwa na mchezaji aliyeingia akitokea benchi Kelechi Iheanacho kufuatia krosi fupi ya Leroy Sane.

Kikosi cha kocha Pep Guardiola kilitawala mchezo katika kipindi cha pili lakini kipa wa Watakatifu Fraser Forster ndiye aliyekuwa kikwazo kwa Man City kufunga.

No comments:

Post a Comment