Tuesday, 20 February 2018

Marubani wa Kenya Waliotekwa Warejea


NAIROBI, Kenya

MARUBANI wawili wa Kenya ambao walikuwa wakishikiliwa na kundi la magaidi Sudan Kusini kwa zaidi ya mwezi mmoja wamerejea nyumbani.

Walitua kwenye Kiwanja cha Ndege Nairobi kabla hawajakutana na ndugu zao.

Rubani Njoki akikutana tena na mtoto wake wakike mwenye umri wa miaka 12, Lucy Muthoni.

Magaidi hao waliwakamata wawili hao mapema mwezi uliopita wakati ndege ilipoanguka katika mkoa wa  Upper Nil, ikiripotiwa kuuwa mwanamke mmoja na baadhi ya mifugo.

Marubani hao wawili waliachiwa juzi kufuatia mazungumzo mazito ya makubaliano yaliyowashirikisha viongozi wa serikali ya Sudan Kusini na wenzao wa Kenya.


No comments:

Post a Comment