Tuesday 13 February 2018

Uefa Yataka Waamuzi Kuwalinda Wachezaji

ZURICH, Uswisi
SHIRIKISHO la Soka Ulaya (Uefa) limewakumusha waamuzi kuwalinda wachezaji kwa kuwapa adhabu kale wale wanaowazea wenzao rafu mbaya katika mashindano ya klabu Ulaya.

Hilop limekuja baada ya kocha wa Manchester City Pep Guardiola kuwataka waamuzi wa Uingereza kuwachukulia hatua wachezaji rafu baada ya Leroy Sane kuumizwa katika mchezo wa Kombe la FA.

Mchezo huo ulipigwa kwenye Uwanja wa Cardiff na ulifanyika mwezi uliopita.
Uefa limewaambia waamuzi kuwa wana kibarua kuwalinda wachezaji katika mchezo wa soka.

"Tunataka wachezaji wacheze, hivyo lazima walindwe, “alisema kiongozi wa waamuzi wa Uefa Pierluigi Collina.

"Hatutaki ifikie mahali hatma ya wachezaji iwe katika wasiwasi kwa sababu ya majeruhi…, “alisema.

No comments:

Post a Comment