Sunday 18 February 2018

DStv Media Bonanza Yafanyika kwa Kishindo Dar

Meneja Uendeshaji wa Multichoice-Tanzania, Ronald Shelukindo (kulia) na Mkuu wa kitengo cha Mawasilinao cha kampuni hiyo, Johnson Mshana wakizungumza na wadau mbalimbali waliofika katika hafla ya DStv Media Day Bonanza Gymkana Club jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu
WAANDISHI wa Habari kutoka vyombo mbalimbali leo walijumuika pamoja katika DStv Media Bonanza lililofanyika katika viwanja vya Gymkana Club Jijini Dar es Salaam.

Katika Bonanza hilo, timu ya soka inayoundwa na wafanyakazi wa DStv na ile inayopundwa na waandishi wa habari kutoka vyombo mchanganyiko (Taswa FC) ziliumana na kutoa burudani safi kwa watu mbalimbali waliofika hapo.
Johnson Mshana akiwa na wadau.
Katika mchezo huo, timu ya Taswa FC iliibuka na ushindi wa mabao 6-2 dhidi ya wapinzani wao hao, ambao walitamba katika kipindi cha kwanza na kushindwa kuendeleza cheche zao kipindi cha pili.

Katika bonanza hilo lililoanza majira ya saa 6:00 mchana hadi 12:00 jioni, washiriki waliburudika na burudani mbalimbali zikiwemo muziki wa dansi `live’ na burudani nyingine.
Pia walipata vinywaji na msosi huku wakibadilishana mawazo baada ya wengine  kutoonana kwa muda mrefu, ambapo hafla hiyo iliwakutanisha waandishi wa vyombo mbalimbali huku DStv ikiahisi kuendelea kushirikiana nao.



Kikosi cha DStv kabla ya kuanza kwa mchezo dhidi ya Taswa FC.

Vikosi vya DStv (wenye jezi bluu) na Taswa FC (nyeupe) kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa kirafki.



Kikosi cha Taswa FC


Mhariri wa gazeti la Dailynews na Sundaynews, Nasongelya Kiyinga akisalimia na mfanyakazi wa DStv, Levina wakati wa hafla hiyo.

Mtangazaji wa SuperSport na mwandishi mkongwe nchini, Aboubakary Liongo akisalimiana na mwandishi wa Mtanzania, Mwani Nyangasa.


Kikundi cha ushangiliaji cha DStv wakati timu yao ilipocheza dhidi ya Taswa FC. Taswa ilishinda 4-2.


Baadhi ya waandishi wakichukua msosi wakati wa bonanza hilo.




Mchezaji wa Taswa FC, Majuto Omary `Bonge' akitafuta njia ya kuwatoka wachezaji wa DStv wakati wa mchezo wa kirafiki wa DStv Media Day Bonanza mapema leo Gymkana Club Jijini Dar es Salaam. Taswa ilishinda 6-2.

No comments:

Post a Comment