Thursday 15 February 2018

DStv Media Day Bonanza Kufanyika Kesho


Na Mwandishi Wetu
BONANZA kubwa la Waandishi wa Habari lintarajia kufanyika kesho Jumamosi katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, imeelezwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shumbana Walwa wa DStv, bonanza hilo litashirikisha Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Katika bonanza hilo kutakuwa na michezo mbalimbali, ambapo timu ya wafanyakazi wa DStv watatoana jasho na timu ngumu ya soka ya Chama cha Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Taswa.
Mbali na mchezo huo na mingine, pia kutakuwa na burudani live ya muziki wa dansi, ambapo wageni waalikwa wataburudika kwa muziki huo kabambe.

Pia waandishi pamoja na wadau wengine wa habari, watapata chakula cha mchana pamoja kuhitimisha shughuli hiyo, ambayo hufanyika kila mwaka.

No comments:

Post a Comment