Thursday 3 August 2017

Multchoice yawazawadia waandishi madishi, jezi katika uzinduzi wa Full Vyenga Bila Vyenga

Mkurugenzi Mkuu wa Multchoice-Tanzania, Maharage Chande (kushoto) akimkabidhi dishi mmoja wa washindi, Abdallah Kaniki katika shindano lililofanyika jana katika viwanja vya DStv kando kando ya barabara ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Katikati ni msanii Rihama Ally
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Multchoice-Tanzania imewakabidhi zawadi zao waandishi wa habari wawili walioshinda ving’amuzi vya DStv baada ya kucheza bahati nasibu.

Waandishi hao, Abdallah Kaniki na Dennis Mpima walipata zawadi hizo baada ya kuchezeshwa bahati nasibu kwa mara ya pili na kuwaibua washindi hao wawili.

Awali, Multchoice-Tanzania waliendesha bahati nasibu, ambapo waandishi wa habari 10 walijishindia jezi za timu mbalimbali za Ligi Kuu ya England na zile za La Liga ya Hispania.

Droo hizo ziliendeshwa wakati wa hafla ya kuzindua vuguvugu la soka ulimwenguni (Full Vyenga Bila Vyenga), ambalo linaanza mwikiendi hii katika nchi tofauti.

Kwa mujibu wa mratibu wa hafla hiyo Shumbana James, Kampuni ya Multchoice kupitia king’amuzi chake cha DStv imezindua kampeni maalum ya Msimu Mpya ijulikanayo kama ‘Full Vyenga Bila Chenga’.
Mwanamke pekee aliyeshinda jezi akikabidhiwa jezi yake na msanii Rihama Ally. Kushoto ni Mkurugenzi wa Multchoice-Tanzania, Maharage Chande.
Alisema Watanzania kupitia DStv watashuhudia mubashara michuano mikubwa ya soka ulimwenguli inayotarajia kuanza hivi karibuni ikiwemo Ligi Kuu ya England (EPL) na ile ya Hispania ya La Liga pamoja na makombe mengine maarufu Duniani.

Pazia la Ligi Kuu ya England litafunguliwa kesho Jumapili Agosti 6 kwa mtanange wa Ngao ya Jamii kati ya Arsenal na Chelsea mchezo ambao utaoneshwa  mubashara kupitia DStv.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa msimu mpya wa soka iliyofanyika katika ofisi za Multichoice Tanzania jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande  alisema kuwa msimu huu wa soka, DStv inawahakikishia wateja wake wote kuliona soka katika muonekano bora zaidi.

Mbali na kuona picha zenye ubora wa hali ya juu, pia Watazamaji watafaidi mechi hizo zikitangazwa kwa lugha ya Kiswahili.

No comments:

Post a Comment