Friday 4 August 2017

Zinedane Zidane ataka kumsajili Mbappe

MADRID, Hispania
MAKUBALIANO kati ya Real Madrid na Monaco kwa ajili ya uhamisho wa Kylian Mbappe yamefifia licha ya Los Blancos baki namatumaini ya kumpata mchezaji huyo.

Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane anasema kuwa watafanya jitihada za kumpata Mbappe endapo klabu hiyo itaamua kumpiga bei Gareth Bale.

Makubaliano yanafanywa ili kiasi cha euro milioni 190 kitolewe ili Real Madrid imchukue mchezaji huyo.

Madrid imeiambia Monaco kuwa wanataka kiasi hicho kipunguzwe ili waweze kumnunua mchezaji huyo.

Kiasi cha euro milioni 222 kiichotolewa na PSG bila shaka kitakuwa kichocheo kikubwa kwa klabu zingine za Ulaya kutoa fedha nyingi ili kumnunua mchezaji nyota.

No comments:

Post a Comment