Friday 4 August 2017

Neymar awaahidi Makombe PSG

PARIS, Ufaransa
NYOTA Mbrazil Neymar ameahidi kuisaidia Paris Saint Germain (PSG) kutwaa mataji baada ya kuingia mkataba wa miaka mitano ya dola za Marekani milioni 264 akihamia kutoka Barcelona.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 akiweka kapuni dola za Marekani milioni 35.5 kwa mwaka mjini Paris lakini alisisitiza kuwa ataonesha thamani ya fedha hiyo.

"Nimefurahi sana kujiunga na Paris Saint-Germain," alisema Neymar.

"Tangu nilipowasili Ulaya, klabu imekuwa moja ya sehemu yenye ushindani zaidi. Na changamoto kubwa kwangu ni kuungana na wachezaji wenzangu wapya….”

"Lengo la Paris Saint-Germain kwa kweli ndio lilinishawishi mimi kutua katika klabu hiyo…Nimecheza misimu minne Ulaya na nina hisi niko tayari kwa changamoto.

"Kuanzia leo, nitafanya kila kitu ili kuwasaidia wachezaji wenzangu, kufungua ukurasa mpya kwa klabu yangu na kuleta furaha kwa mamilioni ya mashabiki dunia kote.”


PSG ilisema kuwa Neymar alitarajia kutambulishwa jana katika Uwanja wa Parc des Princes na leo Jumamosi atatambulishwa rasmi kwa mashabiki.

No comments:

Post a Comment