Monday 7 August 2017

Ronaldo kuikabili Manchester United Super Cup

MADRID, Hispania
NYOTA Cristiano Ronaldo ametajwa katika kikosi cha Real Madrid kitakachocheza mchezo wa UEFA Super Cup dhidi ya timu ya zamani ya mshambuliaji huyo ya Manchester United utakaofanyika Skopje nchini Macedonia.

Mabingwa hao wa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kesho Jumanne watachuana na mabingwa wa Ligi Ndogo ya Ulaya au Europa League huku timu zote zikijaribu kusaka taji la bara la Ulaya kwa mara ya kwanza msimu huu.

Madrid wamemjumuisha Ronaldo, ambaye ndio kwanza Jumamosi alirejea katika mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya baada ya ripoti kuzagaa kuwa mchezaji huyo anataka kuondoka katika klabu hiyo, yumo katika kikosi cha timu hiyo cha wachezaji 24 kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya kocha wake wazamani Jose Mourinho.

Wachezaji wapya waliosajiliwa na timu hiyo, Theo Hernandez na  Dani Ceballos nao pia wamo katika kikosi hicho, pamoja na Ronaldo na wachezaji washambuliaji wenzake, Karim Benzema na Gareth Bale.

No comments:

Post a Comment