Monday, 7 August 2017

TAHA waandaa mashindano ya Nyerere Cup Okt 9-14

Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Mpira wa Mikono Tanzania (Taha) kimeandaa mashindano ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere au Nyerere Cup yatakayofanyika kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa kuanzia Oktoba 9 hadi 14, imeelezwa.

Kilele cha mashindano hayo ndio Siku ya Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Katibu Mkuu wa Taha, Rucy Kiwia (pichani) alisema mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuwa, mashindano hayo yatashirikisha timu za Tanzania Bara na zile za Zanzibar.

Kiwia alisema kuwa wanatarajia mashindano hayo ambayo yatashirikisha jumla ya timu 12, yatakuwa na msisimko mkubwa.

Wakati huohuo, Taha kesho Jumanne Agosti 8 itaandaa bonanza la mchezo wa mpira wa mikono kwa ajili ya maadhimisho ya Nane Nane yatakayofanyika jijini Dar es Salaam.

Aidha, Kiwia alisema kuwa katika kuendeleza mchezo huo chama chake kimekuwa kikiendesha mashindano Mbagala Charambe na kwenye Uwanja wa Ngome jirani na Uwanja wa Taifa kila mwishoni mwa wiki.

No comments:

Post a Comment