Friday 4 August 2017

Liverpool, Hoffenhim kucheza Ligi Mabingwa Ulaya

 LONDON, England
LIVERPOOL itakutana na timu ya Ujerumani ya Hoffenheim katika mbio za kusaka nafasi ya kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

Kikosi hicho cha kocha Jurgen Klopp kitacheza mchezo wa kwanza ugenini kati ya Agosti 15 na 16, huku mechi mchezo wa marudiano ukipangwa kuchezwa Anfield kati ya Agosti 22 au Agosti 23.

Mabingwa wa Scotland Celtic watakutana na wenzao wa Kazakh Astana katika mchezo wa raundi ya mchujo, ambapo mchezo wa kwanza watacheza nyumbani.

Washindi 10 wa mechi za mchujo wataungana na timu 22 ambazo tayari zimeshafuzu kucheza hatua ya makundi.
Timu itakayoshindwa katika raundi ya mchujo zitafuzu kwa hatua ya makundi ya Ligi ya Ulaya.

Liverpool imefuzu kucheza mchezo wa mchujo baada ya kumaliza ya ne katika msimu uliopita wa Ligi Kuu ya England huku Hoffenheim ikimaliza katika nafasi hiyo katika Bundesliga.

Mabingwa Chelsea, Tottenham na Manchester City tayari zimefuzu kucheza hatua ya makundi, huku Manchester United, nayo ikifuzu baada ya kutwaa taji la Ligi ya Ulaya.

Ratiba ya Ligi ya Mabingwa
Qarabag (Azerbaijan) v Copenhagen (Denmark)

Apoel Nicosia (Cyprus) v Slavia Prague (Czech)

Olympiakos (Ugiriki) v HNK Rijeka (Croatia)

Celtic (Scotland) v Astana (Kazakhstan)

Hapoel Beer Sheva (Israel) v Maribor (Slovenia)

Istanbul Basaksehir (Uturuki) v Sevilla (Hispania)

Young Boys (Uswisi) v CSKA Moscow (Urusi)

Napoli (Italia) v Nice (Ufaransa)

Hoffenheim (Ujerumani) v Liverpool (England)


Sporting Lisbon (Ureno) v Steaua Bucharest (Romania)

No comments:

Post a Comment