Tuesday 13 March 2018

Southampton wamtupia Virago Kocha Pellegrino


LONDON, England
KLABU Southampton imemtupia virago kocha wake Mauricio Pellegrino (pichani) huku timu hiyo ikiwa pointi moja na nafasi moja juu ya ukanda wa kushushwa daraja wakati zimebaki mechi nane kabla ya kumalizika kwa msimu.

Watakatifu hao wameshinda mechi moja tu kati ya 17 za ligi zilizopita na ilifungwa mabao 3-0 huko Newcastle United Jumamosi.

Pellegrino, mwenye umri wa miaka 46, aliteuliwa kuifundisha timu hiyo Juni akichukua nafasi ya Claude Puel.

Timu hiyo ina matumaini ya kuwa na kocha mpya kabla haijakabiliana na Wigan Jumapili kwa ajili ya kusaka nafasi ya nusu fainali ya Kombe la FA.

Wako katika msimu wa sita mfululizo katika Ligi Kuu ya England na hawajawahi kumaliza chini ya nafasi ya 14 katika misimu mitno iliyopita.

Pellegrino alisema ameona baadhi ya wachezaji waliokatatamaa wakati wa mchezo wa Jumamosi.

Pellegrino, mcheszaji wazamani wa kimataifa wa Argentina, alipata pointi 0.93 kwa mchezo, ikiwa ni asilimia mbaya zaidi kwa kocha yeyote wa Southampton katika Ligi Kuu.

Klabu hiyo ilisema katika taarifa yake kuwa wanataka kuteua timu mpya ya uongozi haraka iwezekanavyo, tayari hilo liko katika mchakato.

Ni timu ya tisa ya Ligi Kuu kubadili kocha msimu huu.

Kocha msaidizi Carlos Compagnucci na kocha msaidizi wa kikosi cha kwanza Xavier Tamarit nao pia wameondoka katika klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment