Tuesday 13 March 2018

Chelsea Mikononi Mwa Barcelona Kesho Ulaya


BARCELONA, Hispania
KOCHA wa Chelsea, Antonio Conte amesema kuwa timu yake inatakiwa kuteseka hapa kesho ikiwa inataka kufuzu kucheza hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

Barcelona inaikaribisha Chelsea leo katika mchezo wa marudiano wa hatua ya 16 baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Stamford Bridge mjini London.

Chelsea ina kibarua kigumu kwani inahitaji ushindi wa aina yoyote au sare ya kuanzia mabao 2-2 ili kusonga mbele katika mashindano hayo makubwa ya klabu barani Ulaya.

Barcelona ilifunga bao la kusawazisha katika dakika ya 75 kupitia kwa Lionel Messi kufuta bao la kuongoza lililofungwa katika kipindi cha pili na kiungo Willian katika mchezo wa kwanza mwezi uliopita.

Conte alisema timu yake itakabiliana na kibarua kigumu dhidi ya mabingwa hao mara tano wa Ulaya katika mchezo huo utakaofanyika Nou Camp.

"Tunatakiwa kuwa vizuri sana lakini unapocheza dhidi ya timu kama hii, ambayo nafikiri ni moja ya timu bora duniani, lazima ujiandae kutaabika, kama vile tulivyofanya katika mchezo wa kwanza, ambako tulijiandfaa vizuri, alise,a Conte katika mtandao wa klabu hiyo.

"Hii sio ile timu (Chelsea) yenye wachezaji wazoefu ambao wanacheza msimu wa kwanza au wa pili katika Ligi ya Mabingwa.

"Lakini tunatakiwa kucheza kama timu na na kujaribu kuwa tayari kutaabika, na katika kila muda tunatakiwa kujua kuwa tunaweza kuwa na nafasi ya kufunga.

Barcelona ilitawala katika mchezo wa awali, lakini kikosi cha Conte kwa bahati mbaya hakikupata ushindi baada ya Willian mara mbili kushindwa kufunga kabla ya mapumziko.
Barcelona imezidi kuimarika kwa ajili ya mchezo huo baada ya nahodha wake, Andres Iniesta, ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa sababu ya maimivu, juzi alianza mazoezi kwa ajili ya mchezo huo.

Iniesta alifanya sehemu ya mazoezi pamoja na baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Barca, akiongeza matumaini ya kurejea katika mchezo huo wa marudiano wa hatu ya 16 bora.

Iniesta aliumia Barcelona ilipocheza dhidi ya Atletico Madrid siku nane zilizopita na Jumamosi alikosa mchezo walioshinda 2-0 dhidi ya Malaga.

Pia timu hiyo Jumamosi ilimkosa nyota wake Lionel Messi, ambaye alikwenda kushuhudia kuzaliwa kwa mtoto wake, Ciro, lakini mshambuliaji huyo atakuwemo katika mchzo huo.

No comments:

Post a Comment