Thursday 22 March 2018

Heart Marathon 2018 Sasa Kupigwa Aprili 29


Na Mwandishi Wetu
MSHINDI wa kwanza wa mbio za Heart Marathon ambazo sasa zitafanyika Aprili 29 badala ya Aprili 26, atazawadiwa kiasi cha Sh milioni 2.

Akizungumza na waandishi wa habari Mikocheni, Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa mbio hizo, Rebecca John alisema kuwa, wamebadilisha tarehe ya kufanyika mbio hizo baada ya kuombwa na wadau.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Maandalizi ya Mbio za Heart Marathon 2018, Rebecca John (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Mikocheni Jijini Dar es Salaam kuhusu mbio hizo, Kulia ni Mwakilishi wa Riadha Tanzania (RT), Tullo Chambo na Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam (DAA), Lucas Nkungu.
John alisema kuwa lengo kuu la mbio hizo ni kuhamasisha mfumo bora wa maisha unaosaidia kupunguza kuenea kwa magonjwa yasiyoambukiza kama magonjwa ya moyo, kisukari, presha na saratani.

Mbali na mbio za kilometa 21, Heart Marathon pia inashirikisha mbio za baiskeli za umbali huo, zile za meta 700 kwa watoto wenye umri chini ya miaka 12, kimoeta 10 na zile za kilometa tano,
Mwakilishi wa Riadha Tanzania (RT), Tullo Chambo akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu Heart Marathon leo. Kulia ni katibu Mkuu wa Kamati ya mbio hizo, Rebecca John, na Katibu Mkuu wa DAA, Lucas Nkungu.
Akitangaza zawadi kwa washindi kuwa mshindi wa kilometa 21 kwa upande wa wanawake na wanaume, kila mmoja ataondoka na Sh 2 wakati mshindi wa pili Sh milioni 1.5 na yule watatu atapewa Sh milioni 1.

Alisema kuwa zawadi zimeongezwa sana, ambapo katika mbio za mwaka huu mshindi wan ne hadi wa 10, kila mmoja atapewa kifuta jasho cha Sh 100,000 tofauti na miaka ya nyuma, ambapo washindi watatu tu ndio waliokuwa wakipewa zawadi hizo za fedha.

Mbali na kutoa zawadi kwa watakaokuwepo katika 10 bora, pia waandaaji wameongeza zawadi kwa washindi kutoka Sh 500,000 ya mwaka jana hadi milioni 2 za mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam, Lukas Nkungu akizungumza na waandishi kuhusu mbio za Heart Marathon leo Mikocheni, Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Riadha Tanzania, Tullo Chambo alisema kuwa wako tayari kuwasaidia waandaaji wa mbio hizo ili kuhakikisha wanafikia malengo yao ya kuuendeleza mchezo huo nchini.

Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam (DAA), Lukas Nkungu alisema kuwa wako pamoja na waandaaji hao, ambapo aliwaomba watu kujitokeza kwa wingi ili kupima afya zao baada ya kushiriki mbio hizo siku hiyo


No comments:

Post a Comment