Thursday 22 March 2018

Usain Bolt kufanya mazoezi na Dortmund


DORTMUND, Ujerumani
GWIJI wa riadha Usain Bolt, ambaye anania ya kuanza kucheza soka akiwa na umri wa miaka 31, leo Ijumaa ataanza mazoezi na klabu ya Borussia Dortmund , klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani ya Bundesliga imetangaza.

"Bolt anakuja!" klabu hiyo ya Ujerumani ilitwitt wakati mkiambiaji huyo wa mbio fupi wa Jamaica alipoandika "BVB, kaeni tayari kwa ajili ya ujio wangu Ijumaa " aliandika katika akaunti yake rasmi.

Tukio hilo limetangazwa hadharani kufuatia wote Bolt na Dortmund kudhaminiwa na Puma.

Mazoezi hayo yamepangwa kufanyika kuanzia saa 10:30 asubuhi kwa saa za haoa na yatakuwa wazi kwa watu wote huku vyombo vya habari kibao vikitarajia kuripoti tukio hilo.

Bolt, ambaye anashikilia rekodi ya dunia yam bio za meta 100 na 200, alitangaza januari atafanya mazoezi ya soka na klabu ya Dortmund wakati wa mapumziko ya ya kipindi hiki.

Tangu alipopstaafu kukimbia mwaka jana, Bolt hakuficha ndoto yake ya kutaka kucheza soka.

Mashabiki wa Manchester United watajipanga kumshuhudia mwanamuziki nyota wa Pop wa Uingereza Robbie Williams katika mchezo wa kuchangia utakaofanyika kwenye Uwanja wa Old Trafford Juni 10.

Bolt, bingwa mara nane wa medali ya dhahabu wa Olimpiki, ataongoza wachezaji 11 wa timu ya Msaada ya Dunia kwa ajili ya kukusanya fedha kwa Shirika la Kimataifa la Watoto (Unicef).

No comments:

Post a Comment