Saturday 17 March 2018

Wenger Aikwepa Atletico Robo Fainali UEFA Ndogo


ZURICH, Uswisi
KOCHA Arsene Wenger amefanikiwa kuikwepa Atletico Madrid baada ya timu yake kupangwa na CSKA Moscow katika robo fainali ya Kombe la Ligi.

Wenger tangu awali alikaririwa akisema kuwa hataki kabisa kusikia timu yake imepangwa na Atletico Madrid katika hatua hiyo ya robo fainali.

Alisema kwa kikosi hicho cha Diego Simeone kinapewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo mwaka huu.

The Gunners itakuwa mwenyeji wa mchezo wa kwanza utakaofanyika kwenye Uwanja wa Emirates Aprili 5 huku mchezo wa marudiano utapigwa wiki moja baadae mjini Moscow.

Timu ya Hispania ya Atletico Madrid, ambayo inashika nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya Hispania, La Liga, itakabiliana na Sporting Lisbon ya Ureno.
Katika mchezo mwingine, timu ya Ujerumani ya RB Leipzig itacheza dhidi ya Marseille ya Ufaransa, wakati klabu ya Italia ya Lazio itacheza dhidi ya Salzburg ya Austria.

No comments:

Post a Comment