Saturday 17 March 2018

Liverpool, City Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya


ZURICH, Uswisi
LIVERPOOL itamenyana na wapinzani wake wakubwa wa Ligi Kuu ya England, Manchester City katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

Timu hizo tayari zimekutana mara mbili katika Ligi Kuu ya England msimu huu,kila moja ikishinda mchezo wake wa nyumbani.

Uwanja wa Anfield utaandaa mchezo wa kwanza wa robo fainali utakaofanyika Aprili 3 na 4 huku ule wa marudiano utakuwa Aprili 10 na 11.
Man City ilitinga robo fainali baada ya kuifunga Basel kwa jumla ya mabao 5-2, wakati Liverpool iliibwaga Porto kwa mabao 5-0 katika mchezo wa kwanza huko Ureno.

Mabingwa watetezi Real Madrid itakutana na Juventus wakirudia fainali ya mwaka jana, Sevilla imetinga hatua hiyo badaa ya kuitoa Manchester United itakutana na mabingwa mara tano Bayern Munich, wakati Barcelona watakutana na Roma.
Ratiba Kamili ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya:

Barcelona v Roma

Sevilla v Bayern Munich

Juventus v Real Madrid

Liverpool v Manchester City

Mechi za kwanza za robo faiali zitapigwa Aprili 3 na 4 na mechi za marudiano zitapigwa Aprili 10/11.

No comments:

Post a Comment