Tuesday, 20 March 2018

Real, Barca, PSG Wamfukuzia Salah kwa Fedha Nene


LONDON, England
LIVERPOOL inapambana ili kumbakisha mchezaji wake Mo Salah anayetakiwa na klabu kibao kwa ada ambayo ni rekodi ya dunia ya pauni milioni 200.

Real Madrid, Barcelona na Paris Saint-Germain (PSG) zote zinamtaka nyota huyo wa Misri kwa fedha kibao.

Mchezaji huyo amekuwa mpachikaji mzuri wa mabao msimu huu kwa Anfield, ambapo tayari ameshafunga mabao 37 katika mechi 43 alizoichezea klabu hiyo.

Na hiyo ina maana kuwa kocha Jurgen Klopp atakataa ada hiyo ya rekodi ili kuendelea kumbakisha mchezaji huyo katika klabu hiyo.

Salah, ambaye aliigharimu Liverpool kiasi cha pauni milioni 34.3 kutoka Roma katika kipindi cha majira ya joto, akifananishwa na Lionel Messi na bao zake 28 katika  Ligi Kuu ikiwa na maana amefunga mabao matatu zaidi ya ligi zaidi ya mchawi huyo wa Argentina.

Real itatupilia mbali nia yake ya kumsajili Eden Hazard wa Chelsea endapo itamnasa Salah wakati Barca tayari imeshapiga kelele kuhusu Mmisri huyo.

Swali ni je, Liverpool itaendelea kumbakisha Salah au itaweka mbele fedha kama ilivyofanya kwa Coutinho.

No comments:

Post a Comment