Thursday 28 September 2017

Maghembe Kufungua Maonesho ya Utalii Karibu Kusini yanayofanyika Kihesa mkoani Iringa

Mhandisi Kerdick Chawe (kushoto) akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza (mwenye ushungi) kwenye banda la maonesho la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wanaoshiriki kwenye maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika kwenye viwanja vya Kichangani mkoani Iringa.

Na Mwandishi Wetu,Iringa

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe leo Ijumaa  atafungua rasmi maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim, yanayofanyika kwenye viwanja vya Kichangani mkoani Iringa.

Maonesho hayo yenye kaulimbiu ya Utalii Endelevu ni Nguzo ya Uchumi wa Viwanda yanashirika taasisi za serikali, mashirika ya umma na kimataifa zaidi ya 400, ambapo yatamalizika Oktoba 2, 2017, ambapo yanalengo la kuweka uelewa kwa jamii kuhusu umuhimu wa utalii na thamani thamani ikiwa ni pamoja na kuutangaza utalii kwa kuihamasisha jamii kutumia fursa za utalii zilizopo katika kuinua uchumi wa wakazi wa Ukanda wa Kusini mwa Tanzania na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wa Wizara mbalimbali zipo na taasisi zake ikiwemo Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Idara ya Utalii, Wanyamapori, Mambo ya Kale na Misitu na Nyuki, Chuo cha Taifa cha Utalii, Makumbusho ya Taifa, Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Mamlaka ya Usimamizi ya Wanyamapori (TAWA) Mfuko wa Misitu Tanzania  (TaFF).

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw. Richard Kasesela  (kulia) akisalimiana na Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa kilichopo Kata ya Nduli, katika banda la maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), yanayofanyika kwenye viwanja vya Kichangani mkoani Iringa.

Taasisi nyingine ni Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, (TFS)  Taasisi ya Utafiti wa Misitu na Wadau wa Wizara ya Maliasili na Utalii.Wadau wa Sekta ya Utalii kutoka mikoa  ya Nyanda za Juu Kusini watashiriki kuonesha bidhaa na huduma zao muhimu na mikoa inayoshiriki ni pamoja na wenyeji Iringa, Mbeya, Ruvuma, Songwe na Njombe.

Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bi. Bahati Mollel akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Bw. Richard Kasesera katika banda lao la maonesho ya Utalii ya Karibu Kusini yanayofanyika kwenye viwanja vya Kichangani mkoani Iringa.

Fursa zilizopo nyanda za Juu Kusini ni pamoja na Ziwa Tanganyika, Ziwa Rukwa,  Ismila,Kalenga na Boma la Mkuu wa Wilaya, Hifadhi za Mahale, Katavi, Ruaha, Kitulo na Selous.




No comments:

Post a Comment