Friday 8 September 2017

Liverpool yamuweka kando Coutinho ikiifuata City

LONDON, England
KIUNGO Philippe Coutinho (pichani) ameachwa nje ya kikosi cha Liverpool ambacho kesho kitakwaana na Manchester City katika moja ya mechi za Ligi Kuu ya England.

Mchezo huo utapigwa mapema kuanzia saa 8:30 mchana kwa saa za Afrika Mashariki kwenye dimba la Etihad.

Coutinho, 25, amerejea klabuni baada ya mara mbili akitokea benchi alipoichezea Brazil katika mechi za kufuzu kwa Kombela Dunia 2018.

Mchezaji huyo alikosa mechi za Liverpool za mwanzo wa msimu kutokana na maumivu ya mgongo pamoja na kutaka kuhamia Barcelona.

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp alisema: "Nimeamua kutomjumuisha katika kikosi changu kitakachocheza na Man City ili aweze kutumia muda kwa ajili ya mazoezi zaidi. Alikubali.”

Klabu hiyo ilitupilia mbali ofa tatu kutoka kwa vigogo vya soka vya Hispania, Barcelona ambao walikuwa wanataka kumsajili Coutinho – aliyeomba uhamisho, ambapo klabu hiyo ilisisitiza kuwa mchezaji huyo hauzwi.

Alifunga katika ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Ecuador Ijumaa ya wiki iliyopita, na pia aliingia kitokea benchi katika mchezo wa Jumanne walipotoka sare ya 1-1 na Colombia.

Mechi zingine leo zitakuwa kati ya Southampton itakayoikaribisha Watford          kwenye Uwanja wa St. Mary's kuanzia saa 11:00 jioni, huku Brighton & Hove Albion ikicheza dhidi ya West Bromwich Albion.

Everton           wenyewe watakuwa wageni wa Tottenham Hotspur katika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Goodison Park huku Arsenal  itakuwa na kibarua dhidi ya AFC Bournemouth kwenye Uwanja wa Emirates.

Mabingwa wazamani Leicester City watawakaribisha mabingwa watetezi, Chelsea         kwenye Uwanja wa King Power, huku Stoke City watakuwa wenyeji wa Manchester United.

No comments:

Post a Comment