Friday 29 September 2017

Cecafa yaipa Kenya uenyeji Kombe la Chalenji 2017

NAIROBI, Kenya

BARAZA la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki (Cecafa) limeitangaza Kenya kuwa mwenyeji wa mashindano ya Chalenji ya wakubwa, ambayo hayajafanyika kwa miaka miwili sasa.

Kwa mara ya mwisho mashindano hayo ya Chalenji yalifantyika Ethiopia na Uganda ndio ilitwaa ubingwa huo.

Katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya Cecafa kilichodanyika Khartoum, Sudan, wajumbe walionesha msiokamano na Kenya dhidi ya kupokonywa uenyeji wa mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani, Chan Januari 2018.

 

Mashindano  ya wakubwa ya Chalenji yanashirikisha mataifa yote 13 wanachama wan chi za Afrika Mashariki na Kati, yatafanyika Novemba na Desemba mwaka huu.

Uganda ndio mabingwa wasasa wa mashindano hayo baada ya kutwaa kwa ara ya mwisho mwaka 2015 baada ya kuifunga Rwanda 1-0 katika fainali.

Mkutano huo pia ulizitangaa Burundi na Rwanda kuwa wenyeji wa mashindano ya Cecafa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 na yale ya wanawake Novemba na Desemba.

 

No comments:

Post a Comment