Saturday 9 September 2017

Manchester City yaikandamiza Liverpool 5-0

LONDON, England
MANCHESTER City imetoa kipigo cha `mbwa mwizi’ baada ya kuifunga Liverpool pungufu kwa mabao 5-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Etihad.

Ushindi huo ni ujumbe mzito wa Manchester City kwenda kwa wapinzani wake wanaoshindana nao kuwania taji hilo la Ligi Kuu.

Liverpool ilipata pigo baada ya mchezaji wake mmoja Sadio Mane kutolewa baada ya kumchezea vibaya hewani Ederson na kusabbaisha kipa huyo kupata matibabu ya muda mrefu kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Claudio Bravo.


Mabao ya Man City yalifungwa na Agüero katika dakika ya 24, Gabriel Jesus katika dakika ya 45 na 53, Sane katika dakika ya 77 na 90.

Katika mechi zingine leo, Arsenal iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya  AFC Bourne huku Chelsea ikishinda mabao 2-1 dhidi ya Leicester City.

No comments:

Post a Comment